
Tangazo hilo la mgawo ambalo limekuja katika kipindi ambacho mjadala wa jenereta za kampuni ya Dowans ukiwa umeibuka tena, linatarajiwa kuongeza gharama za maisha kutokana na ukweli kuwa viwanda vingi vitalazimika kutumia jenereta katika uzalishaji licha ya Tanesco kutangaza kuwa vitapewa umeme nyakati za mchana.
Wananchi ambao kipato chao kinategemea biashara ya samaki, saluni, na vinywaji pia wataguswa na makali hayo moja kwa moja wakati mabenki, vituo vya mafuta, mahoteli na makampuni mengine ya kutoa huduma yatajikuta yakiingia gharama kubwa katika utendaji wao.
Tangazo la Tanesco limetolewa wakati kukiwa na ahadi kemkem za kumaliza kabisa tatizo la mgawo wa umeme, huku Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ikiwa imeliruhusu shirika hilo la umma kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 18.5.
"Mgawo huu wa umeme umeshaanza kwenye mikoa yote na utadumu kwa majuma manne hadi katikati ya mwezi Januari mwakani," alisema meneja mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alipoongea na waandishi jana.
"Mgawo utahusisha mikoa yote iliyounganishwa kwenye gridi ya taifa isipokuwa mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Kigoma, Lindi na Mtwara."
Kwa mujibu wa Masoud, mgawo wa sasa umetokana na upungufu wa umeme uliojitokeza baada ya moja ya visima vinavyozalisha gesi vya kampuni ya Pan African Energy, kuzimwa.
Alisema kisima hicho kinachotoa gesi kimezimwa kwa ajili ya kukifanyia matengenezo ya kawaida, hivyo kusababisha upungufu wa megawati 40 za umeme zinazokwenda katika gridi ya taifa.
Pan African Energy ni kampuni ambayo inachimba gesi hiyo eneo la Songo Songo, Kilwa na baadaye husafishwa na kusafirishwa na kampuni ya Songas ambayo huzalisha umeme wa megawati 180 eneo la Ubungo na kuiuzia Tanesco.
Kwa mujibu wa makubaliano, Songas hutakiwa kuzalisha umeme kwa kiwango kilicho kwenye mkataba na ni jukumu la Tanesco kuutumia umeme huo wa gesi kulingana na mahitaji yake au kutoutumia. Tanesco huilipa Songas hata pale inapokuwa haitumii umeme wa kampuni hiyo.
Badra alisema kuwa kiwango hicho cha upungufu wa umeme kinaweza kuongezeka hadi kufikia megawati 120 jambo alilosema likitokea, shirikma hilo litazidisha mgawo.
“Wakati mwingine kunapokuwa na peak (matumizi yanakuwa makubwa), upungufu unaweza kufikia megawati 120. Ikitokea hivyo, kwa kuwa sasa tunategemea uzalishaji umeme kwa njia ya maji, itabidi nasi tuongeze mgawo,” alisema Badra.
Alieleza kuwa mgawo huo utaanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni katika baadhi ya maeneo huku maeneo yaliyopata umeme katika muda huo yakiukosa kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku mara tatu kwa wiki.
Kwa mujibu wa Badra, ratiba ya mgawo huo zitatangazwa katika magazeti na vyombo vingine vya habari.
Hata hivyo, alisema baadhi ya maeneo hayatakumbwa na mgawo huo akitaja baadhi kuwa ni hospitali, pampu za maji, migodi na viwandani ambako alisema vitakosa umeme usiku ili mchana viendelee kuzalisha.
Alisema kuwa maeneo yanayopata umeme kutoka transoma ya Kipawa hawatakumbwa na mgawo huo, kutokana na kukamilika kwa matengenezo yake.
“Transfoma ya Kipawa imeshatengemaa na hivyo kuanzia Desemba 23 (jana) haki ya kupata umeme katika maeneo yaliyoathirika kutokana na kuharibika kwa transfoma hiyo, itarejea kama kawaida na wateja wa maeneo hayo hawatakumbwa na mgawo huu tulioutangaza,” alisema Badra.
Baadhi ya maeneo yanayopata umeme kutoka transfoma hilo ni pamoja na Yombo Dovya, Tandika, Temeke, Chang’ombe, Chamazi, Tazara, Maji Matitu, Charambe, Keko na Uwanja wa Taifa.
Akizungumzia siku kuu za Krisimasi na Mwaka Mpya, Badra alisema Tanesco itajitahidi kuhakikisha wananchi wanasherehekea siku hizo bila kukosa umeme huku akiwaomba radhi kwa mgawo huo.
Mgawo wa umeme, ambao ulizalisha kashfa kubwa ya Richmond ulipoibuka mwaka 2006, umeshaanza kuzoeleka kwa wananchi na ahadi za shirika hilo na wizara kugeuza tatizo hilo kuwa historia, sasa zinaonekana za kawaida.
Machi 16 mwaka huu Tanesco ilitangaza mgawo wa umeme katika mikoa yote ya Tanzania Bara uliokuwa wa saa tano kila siku. Wakati mgawo huo ukiisha, Tanesco ilitangaza kuwa tatizo la umeme sasa litakuwa historia.
Watanzania, ambao ni asilimia 12 tu wanaotumia huduma hiyo majumbani, pia walipata machungu ya mgawo wa umeme Oktoba mwaka uliopita ambapo walikosa huduma hiyo kwa saa 12 kwa siku.
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo Stephen Mabada, alitangaza mgawo huo akieleza kwamba Tanesco ililazimika kuanza mgawo huo kutokana na upungufu mkubwa wa uzalishaji umeme, uliosababishwa na kuharibika kwa mitambo minne kwenye vituo vya uzalishaji wa nishati hiyo.
Mitambo iliyoharibika ilikuwa ni ya Kidatu, mkoani Morogoro, Kihansi (Iringa) na Pangani (Tanga) wakati jijini Dar es Salaam mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi asilia wa Songas pia uliripotiwa kuharibika.
Wakati huo, serikali iliamuru kuwashwa kwa mitambo inayozalisha umeme kwa kutumia mafuta ya IPTL licha ya kampuni hiyo na Tanesco kuwa kwenye mgogoro mkubwa ambao unashughulikiwa mahakamani.
Matatizo makubwa ya umeme yaliibuka mwaka 2006 wakati nchi ilipokumbwa na janga kubwa la ukame na ikabidi serikali ichukue hatua za dharura kumaliza tatizo hilo.
Lakini hatua hizo za dharura zikaishia kwenye kashfa kubwa ya utoaji zabuni ya uzalishaji umeme kwa kampuni ya Richmond Development LLC, ambayo ilidhihirika baadaye kuwa haikuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wake kwenye mkataba.
Baadaye mkataba huo ulirithishwa kwa kampuni ya Dowans Tanzania ambayo, licha ya kuchelewa, ilileta nchini mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi iliyokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 120.
Lakini mwaka 2008 Tanesco ilikatisha mkataba huo mwaka mmoja kabla ya kumalizika, ikidai kuwa Sheria ya Manunuzi ya Umma ilikiukwa wakati wa kuingia mkataba huo, lakini ikaahidi kuwa ina uwezo wa kuzalisha umeme bila ya kutegemea jenereta hizo.
Uamuzi huo uliifanya Dowans kufungua kesi Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC), ikidai kuwa taratibu hazikufuatwa wakati wa kuvunja mkataba huo.
Mwaka mmoja baadaye Tanesco ikaibuka na hoja ya kutaka kuinunua mitambo hiyo ya Dowans, ikidai kuwa nchi ilikuwa hatarini kuingia kwenye tatizo kubwa la umeme na kwamba isingekuwa rahisi kununua mitambo mingine kabla ya tatizo hilo kuanza.
Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa vikali na Kamati ya Madini na Nishati ambayo ilieleza kuwa kununua mitambo hiyo mitumba ni kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma, kitu kilichomfanya mkurugenzi wa Tanesco wa wakati huo, Dk Idris Rashid kutoa tamko kuwa iwapo nchi itaingia gizani, asilaumiwe.
Mapema mwezi huu, ICC) ilitoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Dowans na kuiamuru Tanesco kuilipa kampuni hiyo binafsi fidia ya Sh185 bilioni.
Source: www.mwananchi.co.tz
hivi haya mambo mpaka lini jamni tumechoka sasa badala ya kwenda mbele kila siku tunarudi nyuma hivi hawa viongozi wanafanya nini jamani hili ni tatizo kubwa kweli "jamani jueni kula na vipofu"ningeshauri japo dar isikumbwe na mgao maana ni mji unaoleta pato kubwa sana kwa taifa.
ReplyDeletejamani mlokuwa nje ya Tanzania msirudi , sisi tunataka kutoka ...
ReplyDeletekama tuko HELL
Wadanganyika hoyeeee....!!
ReplyDeleteanko pole kwa giza litakalokukumba..samahani lakin naomba kuuliza..hivi hako kahuduma ka'umeme mnapewaga bure nini huko bongo??
Jamani Mh.Dr. JK alipoingia madarakani tu tatizo la kwanza alilokumbana nalo lilikuwa hili la umeme, miaka mitano imepita hali inazidi kuwa mbaya zaidi.Yani hii ilikuwa ni kigezo tosha cha kunyimwa kura za uraisi,na ni wazi kuwa hali itazidi kuwa mbaya hivi hivi hapo atakapomaliza muda wake, hadi hapa mimi napiga kura ya kutokuwa na imani naye!!
Jamani sasa kama ni 12% tu ya waTZ mil.43 ndio wanatumia huduma ya umeme (yani watu wasozidi mil.6) na bado nchi inashindwa kuhudumia huduma hii muhimu ktk maendeleo, je itakuwaje hapo wananchi watakapoendelea ambapo kila mmoja atataka atumie huduma hii..!!
Yani mimi nasikitikaaa...nakosa pa kutokea..!!!
MVP
Bongo tambalaleeee...
ReplyDeleteSOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR,SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR, SOLAR
ReplyDeleteumebana meseji yangu eeh?? hata ukibana vile watu wasishtukie dili we vipi my wife wako ni bomba leta ile picha huku mbona umebania ile picha? au mgao umeanza kukuletea hasira pole sana bongo tambarare ccm oyeeeeeeeeeee, maisha bora kwa kila mbongo na mbadoooooooo
ReplyDeleteanony wa 05.59 pm umenichekesha na kunisikitisha at the same time..kwa mtaji huu harudi mtu, tutaendelea kubanana na wazungu kwenye nchi zao hadi kiama..
ReplyDeleteR I P TANZANIA.
ReplyDeleteJamani tumechoshwa na mambo ya aibu kila siku,sijui yataisha lini??ingetafutwa solution kamili ya kutatua tatizo hili sugu,na ni kwa nini Tanzania tu???Nchi kama Rwanda,Uganda,Kenya nk.mbona hazina mambo haya??Tena ukiangalia Uganda na Rwanda wamekuwa na vita mara kwa mara lakini sasa wanaelekea kutupita.Inabidi watanzania tuwe makini tunapotetea na kucahagua viongozi wabovu,wakati wa kampeni wanakuwa na midomo mitamu,wakishachaguliwa tu,shida sugu zinaendelea kama kawaida !!!sijui kama nchi yetu ililaaniwa au la??Hii ndiyo inafanya baadhi yetu kuogopa hata kurudi huko bongo ingawa tunai miss sana nchi yetu,Tunaposikia habari kama hizi na ufisadi uliokithiri ktk serekali yetu basi tunaona heri tuzeekee huku huku ugaibuni kusikokuwa na mambo ya hovyo kama haya.Sasa imagine kama umeme utakuwa wa mgao namna hiyo kwa mwezi mzima kutakuwa na maendeleo hapo??au ni kudanganyana??Itakuta pengine kuna kiongozi fulani serikalini ana mpango wa kufanya biashara ya generators ndiyo kunakuwa na hali kama hii!!Tukumbuke wakati wa speed govenor kwenye vyombo vya usafiri,je zoezi hilo liliishia wapi???Hakuna nchi ya ki afrika ambayo wananchi wake wanateseka kama Tanzania,pamoja na kujisifu kuwa tuna amani,mimi sioni hata maana ya kuwa na amani hiyo,kila siku shida tupu.
ReplyDeletemdau Usa.
KWA KWELI TAIFA LETU LIKO KWENYE WAKATI MGUMU SANA, NA WANACHI WATAENDELEA KUTESEKA BILA KUPATIKANA KWA UVUMBUZI WA MATATIZO MAKUBWA KAMA HAYA.HUWA HATA MTOTO ALIYE SHULE YA MSINGI ANAWEZA KUONA KWAMBA KUNA TATIZO HAPA;ACHILIA MBALI VIGOGO WANAOPEWA NYADHIFA ZA KUONGOZA WANANCHI NA KUSHUGHULIKIA MATATIZO YAO.HIVI HAWA VIONGOZI WANAOINGIA KWENYE HII MIKATABA YA MITEGO HUWA WANATIA SAHIHI WAKIWA WAMEWEKEWA BASTOLA KICHWANI?AU WANATIA SAHIHI HII MIKATABA WAKIWA WALEVI?AU WANATIA MIKATABA WAKIWA GIZANI KWAMBA HAWAKUPATA KUSOMA NA KUELEWA?HII HAIHITAJI KUWA NA STASHAHADA KUTAMBUA KUWA KUNA TATIZO HAPA.SIELEWI WATU WANAOPPEWA DHAMANA NA WANANCHI WANAZITUMIAJE;WAKUMBUKE KUWA UONGOZI NI WITO NA WATAKUJA ULIZWA NA MAMLAKA INAYOGAWA VIPAJI SIKU MOJA. HIVI VILIO VYA WATU WASIO NA UWEZO WA KUBADILISHA MAMBO YANAYOWAKERA HAVIWEZI KUISHIA TU HEWANI;MACHOZI YAO NA MALALAMIKO HUWA YANASIKIKA NA ANAYESIKILIZA VILIO VYAO HUWA ANATOA ADHABU KWA NAMNA NYINGI;HIVYO KAMA KUNA ALIYEPEWA WADHIFA NI VEMA AKAUTUMIA KIMAADILI.
ReplyDeleteTUSAHAU KITU KIITWACHO MAENDELEO KAMA KILA MWAKA TUNAKUMBANA NA MGAWO WA UMEME.
HAKUNA NCHI ISIYOKUWA NA SKENDO,LAKINI KWA KWELI TANZANIA TUMEZIDI.TUNAKUWA KWENYE HABARI KWA TAARIFA ZISIZOVUTIA HATA KIDOGO.WENZETU WAKENYA WAMEKUJA NA MKAKATI WA KUJENGA BARABARA ZA NAIROBI,PROJECT KUBWA SANA ITAKAYOIFANYA KENYA IWE KITOVU CHA BIASHARA KWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI,WANAJENGA FLY-OVERS NA KUBORESHA MIUNDOMBINU.SISI TUNAJIKUTA TU KILA SIKU NI KUZUNGUMZIA MGAO WA UMEME,FOLENI,RUSHWA NK NK NK, HUKU HATUJI NA NAMNA YA KUTATUA HATA TATIZO MOJA ZAIDI SANA NI KUKUZA LILILOKUWEPO KUTOKA GRADE MOJA NA KULIPANDISHA GRADE YA JUU.MFANO MZURI NI HUU;MIKATABA INASAINIWA, INAVUNJWA,FIDIA ZINALIPWA, WANANCHI WANABEBESHWA MZIGO.TUMETATUA NINI HAPA?KWA KWELI TUNAPIGA HATUA MOJA MBELE, TISA NYUMA;MAENDELEO SIFURI.
NA VIONGOZI WALIO KWENDA SHULE WAMECHAGULIWA,WANASHERIA WALIOBOBEA WAPO NCHINI, NA VIFUNGU VYA KUWALINDA VIPO;ILA HAKUNA ALIYE TAYARI KPAAZA SAUTI KWA AJILI YA MNYONGE; LA KWANZA NI KUJALI MFUKO BINAFSI KWANZA.NAMNA HII HATUTAFIKA.
Hii propaganda ya kwamba Tanzania imeendelea kuliko Kenya ni uongo mtupu. Asilimia 12% ya watanzania wanaishi kwenye umeme wa mgao. Binafsisha kila kitu na serikali ijiondoe kabisa kwenye biashara ya aina yoyote. Kilimo, viwanda, elimu na shughuli nyingine zimeishinda serikali. Siasa za ujamaa hazitatufikisha popote kwani miaka 49 lakini bado umaskini unaongezeka.
ReplyDeleteWatu badala ya kujadili tatizo wanajadili nini sijui, yaani wanajidili upatikanaji wa umeme? Sijaona hata comment moja inayosema PANAFRICA waadabishwe kwa kushindwa kutimiza wajibu wao. Kuzima kisima kwa mwezi mmoja mzima sio general maintanance kuna tatizo hapo, inaelekea hawa jamaa huwa hafanyi maintanance kila inapotakiwa kufanywa kulingana na taratibu za kitaalamu. Na inawezekana kabisa kuwa kuna chombo kimeharibika ndio inabidi mwezi huo mzima uhitajike kwa maintanance kwa ajili ya kusubiri kikatafutwe na kinunuliwe kiletwe hapa nchini. Hawa PANAFRICA wanajua kuwa hivyo visima si mali yao ni mali ya TPDC na mkataba wao ukiisha wao wanaanza mbele, Je kwanini TPDC hawakuwa wanawabana watu waliongia nao mkataba kuhakikisha kuwa maintance inafanywa kwa wakati unaotakiwa na ambayo haitasababisha mgao mkubwa kama huo utakaoitingisha uchumi wa nchi. Hawa wasipoadabishwa basi hali ndio itakuwa hivyo kila siku.
ReplyDeleteHili la kuwalaumi Tanesco ni kuwaonea hapa walio sababisha yote haya ni TPDC kwa kushindwa wao na washirika wao kuhakikisha kuwa gesi inaflow inakotakiwa. Na je viwanda vinavyotumia gesi vitaadhirika namna gani na nani atawalipa fidia hao wenye viwanda kwa hasara watakayoipata? Ni wakati muafaka sasa kutafuta vyanzo vingine vya nishati na kwa kuwa wawekezaji hawakwepeki ni lazima kuwa na ushindani na mikataba inayowabana wawekezaji ili wasijione wako peponi, wakikosa waachiwe, tukiwakosea watushtaki kwenye mahakama za kimataifa na fidia juu tuwalipe, inabidi tuamke wakikosa na sisi tuwe na nguvu ya kuwadai fidia kwa makosa yao!
Tanesco wao huwa hawana planning unit? Maana kama ingekuwa ni ermegency inaeleweka kwani hata heathrow ilifungwa kwa ajili ya hali ya hewa, lakini hili la maintanance kwani hawana ratiba ya wabia wenzao ya uzalishaji na maintanance wakawa wamejiandaa kwa wakati kama huu?
Hebu tufike mahali umeme uwe biashara na si huduma ya jamii kama ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika, ili uzalishwe na ununuliwe kama bidhaa nyingine yoyote tunayonunua halafu tuone kama kutakuwa na makelele yote hayo. Maana hata hao wanaopiga kelele kuwa wako nje na wanapata umeme muwaulize wanalipa kiasi gani umeme na gesi kwa mwezi, na biashara au huduma ya jamii. Na once ukiwa ni umeme wa biashara huyo mwenye biashara yake atakuwa makini na hatataka awe anapata hasara kwa mgao usio na ufumbuzi. Let us be serious now umeme uwe ni bidhaa kama bidhaa nyinginpia tujue kuwa utakapopatika umeme wa kiulaya ulaya hakutakuwa na Kishoaka wala Kijembe! Na huyo atakayekosa kumpelekea mteja wake nishati ya kuzalisha umeme atakiona cha moto kwa fidia!
Hivi ilikuwaje tatizo hili limeibuka na kuwa kubwa mara baada ya uchaguzi?
ReplyDeleteBadala ya kuondoa tatizo la umeme tulinunua rada kwa vijisenti.
Ile bakaa vipi, ishaletwa tutafutie vyanzo vya umeme?
Daah hii kweli kiboko, wakati States wanaanchi wapo Unemployed na wanagombania kununua $200 Jordan ,Bongo wananchi wanafanya kazi hata Umeme hawana! inabidi Wadanganyika waamke .
ReplyDeleteVITU MUHIMU VINAVYOWEZA KUENDELEZA NCHI HARAKA NI UMEME,MFANO TUKIPIGA MAHESABU MUDA WOTE HUO AMBAO UMEME UTAKOSEKANA NI VIWANDA VINGAPI VITAPUNGUZA UZALISHAJI WAKE, NA NIWATANZANIA WANGAPI WATASIMAMISHA BIASHARA ZAO KWA KUKOSA UMEME, HIVI VYOTE VINGESAIDIA KUINUA NCHI YETU KWA HARAKA LAKINI BADALA YAKE TUNARUDI NYUMA,OOOH!.
ReplyDeleteMARA MGAO HAKUNA TENA,MARA TANZANIA ITASAHAU MGAO,MARA MGAO UTAKUA HISTORIA,ANKO KILA ALOANDIKA KWA HERUFI KUBWA UJUE ANA HASIRA NA VIONGOZI WATU WANAUMIA NDIO MAANA WANATOA MSISITIZO,,,VIONGOZI WAACHE KUTOA AHADI WASI TALK THE TALK WA DO THE DO SIO,KILA SIKU TUAFANYA HILI KUTENDA HAWATENDI HADI LINI?..HAO MAFUNDI WANOUNGUZA MITAMBO KILA SIKU HAWAKUSOMA? HAWAJUI KIWANGO CHA KWH MAXIMUM YAKE AU VIPI? AU WANABAHATISHA TU,HIYO NI HASARA KILA SIKU KWA TAIFA
ReplyDelete