Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Barnaba akiwapa vitu roho inapenda wakazi wa Zanzibar waliofika kwa wingi katika tamasha dogo la filamu (Mini ZIFF) linaloendelea kufanyika ndani ya viwanja vya ngome kongwe,Zanzibar.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Marlow akikirudi Kiduku huku mashabiki wakishangilia kwa wingi,usiku wa kuamkia leo wakati wa ufunguzi wa tamasha dogo la ZIFF,visiwani Zanzibar.
Msanii wa kizazi kipya,Linah nae aliliangusha sebene la kufa mtu wakati wa ufunguzi wa Tamasha Dogo la ZIFF visiwani Zanzibar usiku wa kuamkia leo.
Dogo Dito akipagawiwa wakati kwa kukaribisha mwaka mpya wa 2011.
Shangwe za kukaribisha mwaka mpya 2010 zilitawala ilipotimu saa sita na dakika moja,ndani ya viwanja vya ngome kongwe,Zanzibar.

Kwa Picha Zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Masikini Zanzibar yetu!!!

    ReplyDelete
  2. michu tafadhali huwe unapitia unacho kiandika huu mwaka mpya ni 2011 sio 2010 tena

    ReplyDelete
  3. Ushauri wangu kwa bwana mdogo Marlaw - angalia unachokula na fanya mazoezi ya kutosha maana naona huo mwili unaongezeka kwa kasi ya kutisha. Huyu ninayemuona siku hizi ni tofauti kabisa na yule Marlaw wa 2007.

    ReplyDelete
  4. ahh iwapi zanzibar yetu?

    ReplyDelete
  5. Zanzibar yenu akina nani??? Zanzibar yetu sote acheni hizo...
    Mimi

    ReplyDelete
  6. mdau wa Sun Jan 02, 04:57:00 AM mbona unajigonga? mimi nimesema zanzibari yetu nawewe unauliza yenu akina nani? halafu papo hapo unasema zanzibar yetu sote, huoni kama unajigonga mwenyewe hapo?

    Anyway kukujibu suali lako ni kuwa zanzibar ni ya wazanzibari, mtoto wa kambo hawi wako hata akikwita baba au mama! Mali ya kuiba si yako hata kama ukipita ukiimba kuwa ni yako!

    ReplyDelete
  7. ndugu yangu zanzibar yetu imekwenda arijojo ilobakia ni maumivu tu ya kumbukumbu za enzi za zanzibar ya kweli!!!

    ReplyDelete
  8. Mimi nadhani kwa sasa tusizungumzie suala la serikali 3 kwenye katiba yetu m,pya bali tufikirie kuiruhusu Zanzibar kuwa nchi huru ili tuachane na kadhia za muungano bandia ambao umeshindikana kwa zaidi ya miaka 40 sasa. Tanganyika itaendelea kushirikiana na Zambia kama jirani mwema na katika EAC kama nao wataamua kujiunga.

    ReplyDelete
  9. pity, ningetaraji kuona akina dada/mama waliovaa nadhifu, mavazi ya heshima na shungi ama nywele nadhifu, na akina kaka/baba wenye mavazi nadhifu ya kiafrika wakiimba midundo yetu ya taratibu huku wakisindikizwa na ala mbalimbali za muzuki...inauma sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...