

Mweka hazina katika kikundi hicho,Elsi Sebastian akikabidhi fedha zilizochangwa na wadau mbali mbali waliopo katika kikundi hicho ili kuwasaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu waliopo katika kituo hicho cha Friends Of Don Bosco,kilichopo Kimara Suka,kwa mlezi wa Kituo hicho.

Mwanamitindo,Rihama Burhan akiwakabidhi baadhi ya watoto wa kituo hicho mifuko yenye pea kadhaa za kandambili ikiwa ni sehemu ya misaada hiyo.

Wadau wa kikundi cha REACH OUT, SPEAK OUT AND FIGHTING HIV/AIDS TOGETHER kinachoendelezwa na baadhi ya wadau waliopo ndani ya mtandao jamii wa FaceBook wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa kituo hicho wakati wa kukabidhi misaada hiyo leo.
kwa picha zaidi
BOFYA HAPA
kwa picha zaidi
BOFYA HAPA
Jamani watanzania tupo katika ulimwengu wa ushindani. Kitu kimoja ningependa kuwakumbusha ni kwamba, ukiwa kwa wachezaji vaa kama wao, ukiwa kanisani vaa za kanisani, ukiwa na watoto vaa za kuwafunza. Sasa hizi zinazoonyesha nje ile dhakula ya watoto kwa watoto wadogo wanaokuwa wanaona ndio hulka inayotakiwa. Haya tu nawausia.
ReplyDeleteMimi taona TZ tumejijengea tabia ya kutibu maradhi kuliko kuziua. Hawa wtoto yatima hata zamani walikuwapo lakini kwa kuwa walifunzwa tabianjema waliweza kulelewa na kila mtu. Siku hizi kwa kuwa watoto yatima wamechukuliwa kama mayai , nao wakajiona mayai kweli, hawaaambiliki. ukimgusa tu... oh unaninyanyasa kwa kuwa mie ni yayima.
ReplyDeleteKatika kutoa misaada kwa hawa watoto tuwafunze vile vile kuheshimu walezi..na tatizo la vituo vya yatima litapungua kama si kuisha kabisa.
Ambao wngekuwa walezi wanawaogopa watoto hawa kwa kukwepa lawama. Kumbe TZinashindwa kujua kuwa hata hiyo misaada inaishia modomoni kwa wenye meno.
Namshukuru aliecomment hapo mwanzo, kwa kusema ukweli huyo dada aliyevaa cappelo kwa kweli ametia aibu, anategemea kuwafundisha nini hao watoto ange vaa mavazi ya kujistili kidogo angependeza tu sasa hivyo alivyoo si watoto wanaweza kumkimbia? she looks like a Scarecrow
ReplyDeletetabia ya kutoa msaada kwa yatima kwa njia ya publicity ni kuwa zalilisha yatima hao ni vizuri kutowa misada kwao sasa picha nyingi za nini,mkitoa na mkono wa kulia wa kushoto usione na baraka tele mola ata wajalia.
ReplyDeleteDu! watu mna macho, mie sikuona mpaka niliposoma komenti ndio nikaona.
ReplyDeleteBaada ya hapo nawapeni pongezi kwa moyo wa kusaidia wanaohitaji msaada.