Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. kweli maana wabongo huwa hawazikati, inasikirisha kuona mtu wa maana na lebo yake ya suti kaicha tu hajaikata

    ReplyDelete
  2. na hawaachi kuyavaa iyo milebo,wanaume wengi vilaza sana!!
    yani nikimuona mtu kavaa ivo disqualified apo-apo!

    ReplyDelete
  3. we anony wa Tue Jan 18, 11:02:00 AM 2011
    Nunua ya kwako ukate . Sisi tunaovaa tuachie lebo zetu . kwanini waliozitengeneza wameziweka?

    ReplyDelete
  4. label 2??!!! Jamani naomba nieleweshwe; inamaana uondoe moja au uondoe zote kabisa??!!!
    Niliwahi kumshauri mtu mmoja aondoe label, akasema ndo urembo wenyewe??!!! Kumbe kuvaa na label in ushamba...heheh! basi wako wengi washamba!

    ReplyDelete
  5. Tena hata zinazoshonwa na mafundi mitaani wenye suit wanaomba wawekewe lebo! Utawataka? Nilishajiuliza sana kuhusu hili sikuwaelewa kabisa!

    ReplyDelete
  6. UTAJUAJE KAMA NIMEPIGA KITU CHA DESIGNER??

    ReplyDelete
  7. Sasa nikitoa utajuaje kwamba nimevaa suti ya CUCCI?

    ReplyDelete
  8. suit zenyewe midosho tu.na kwasababu wanajua midosho wanaacha lebo labda watu watakubali..

    ReplyDelete
  9. Yaani inaudhi kuona mtu wa heshima anajirusha na label zake kweli wanaudhi hahahaaaa..., bora tuwaelimishe ...

    ReplyDelete
  10. suti yakooo jamani mtu akitaka kufanya chochote afanye anavyotaka

    ReplyDelete
  11. Lebo zangu mimi SIZITOI NIMEZOEA HIVYO. Hata huku ulaya naona wengi tu wanavaa hivyo hivyo!! Na hao watengenezaji ni kwanini waziweke hizo lebo hapo in the first place!? IT DOESNT MAKE SENSE!! Au sababu ni wazungu tu basi na sisi tufuate!? Msikubali kupelekwa puta. When u use YOUR money do what is comfortable to YOU. Hata kuchomekea suti chomekea tu....

    ReplyDelete
  12. Iwe unavaa na lebo au huvai na lebo, kama mshamba utakuwa mshamaba tu, kama mjanja utakuwa mjanja tu, kama mbumbumbu utakuwa mbumbumbu tu, msomi utakuwa msomi tu, namaanisha wanaosema kuwa ukivaa na lebo unashushsa heshima, nataka kuwaambia kuwa heshima haipimwi na lebo za suti, etc.
    Mbona watu wakivaa jeans, say levi's, wrangler, lee, kwaninini hawatoi zile lebo za kigozi kwa juu nyuma? Nyie mnaojadali hili hamjiulizi? Halafu hii issue inajadiliwa na watanznaia tu sijui ni kwamba watanzania ndo wanajua zaidi ya wengineo au lah??

    Chukulia mfani wa jeans tu nilioutoa hapo juu, kutoa au kutokutoa ni uamuzi wa mtumiaji, mwangaliaji haikuhusu. Kama una suit yako toa au hata weka maua no one will care.......

    ReplyDelete
  13. Mtoto wa mkulima Dar.January 18, 2011

    Ni lazima kuwafuata wazungu katika suala la suti kwani wao ndio wagunduzi wa hizo mnazovaa hilo ndio tatizo. Poleni sana wavaa suti, maana zinawatoa ushamba. waswahili wanasema "ukipenda boga penda na ua lake". Bora ya mie na mgolela wangu aah natanua tu town sina khofu wala shaka ya lebo's or whatever. Thanks nawakilisha.

    ReplyDelete
  14. nashukuru kwa kunielimisha mie nilikuwa nazikazia uzi na kuzipiga pasi

    ReplyDelete
  15. hahahaha mdau hapo juu umenikuna sana, eti kama ukitaka kuchomekea suti chomekea tuu. kama lebel haitakiwi kwanini ziliwekwa pale? si wangezificha? lebel sitoi na suti navaa vile vile. si yangu kwani yenu??????

    ReplyDelete
  16. Hiyo kitu ilinitokea Marekani, mzungu kwenye mnuso aliniuliza mbona bado una label kwenye suti? utarudisha suti dukani baada ya party? Sio kwamba nilikuwa sijui isipokuwa nilikuwa nimevaaa suti mpya na nimesau kuondoa hizo label. Ondoa label kabla ujavaa suti yako, isije tokea aibu kama ilivyonitokea.

    ReplyDelete
  17. Ni ushamba uliotukuka kuvaa suti na label, hilo halina ubishi. mume wangu hawezi kuvaa hivyo asilani, ninaziondoa mwenyewe hata iitwe boss, gucci ondolea mbali. kama ni kwaliti inaeleweka tuu.ila washamba huwa ni wabishi sana mnaiga kuvaa suti mkirekebishwa mnakuja juu,
    KWELI USHAMBA MZIGO!!

    ReplyDelete
  18. NA WALE WANAONUNUA MAGARI WATOE LEBO ZA DEALERS. MNALIPWA KUTANGAZA HIZO BIASHARA? AU MMEPEWA BURE HAYO MAGARI? ARE YOU PROUD OF DRIVING A USED CAR? BORA ZINGEKUWA LABEL ZA MAKERS KAMA TOYOTA MAANA TUNGEJUA GARI NI MPYA. MNANIBOA SANA GARI MPAKA INACHAKAA MNAENDELEA TU KUTANGAZA BIASHARA ZA WATU BURE.

    ReplyDelete
  19. Nimependa hiyo ya kuwasema hao wasotoa lebo za used car companies kwenye magari yao. Huwa najiuliza hayo magari ni ya kampuni za kuuza hizo used car au? Jamani hamuoni kama ni uchafu kuacha lijikaratasi la biashara kwenye gari lako. Kama vipi ombeni mlipwe kutangaza biashara zao. POLENI kwa ulimbukeni.

    ReplyDelete
  20. Jambo, lebo zinawekwa paleili iwe rahisi kuijua ikiwa imetundikwa kule dukani kwa ajili ya easy selection ya designer! no wonder wameshikiza na single uzi.
    hizo lebo za magari si mchezo na ikiwa mpya na lastik karatasi zake kabisa., vipi zile za TV,friji, radio. ni rha kamili.

    ReplyDelete
  21. Du ya leo kali,binafsi naishi Canada,lakini kusema kweli kila ninunuapo suti zangu kazi ya kwanza nikishajipima na kuona iko fit jambo la kwanza nikutoa hizo lebel,watu wengi wenye heshima zao huwa siwaoni wakiwa na suti zenye lebel,nijuavyo ukiingia kwenye hizi Mall kubwakubwa ni rahisi kunagalia lebel kwenye mikono ya suti badala ya kutoa kwenye hanger,na kama nikutaka watu wajue umevaa suti ya bei mbaya mbona hata chupi jamani tunavaa za bei mbaya lakini wewe mwenyewe mvaaji ndo unayejua kuwa umevaa chupi ya bei mbaya,hata mie kwakweli nadhani ni ushamba tu.

    ReplyDelete
  22. we mdau unaesema kuhusu chupi za bei mbaya.. kwani huonagi mtu akivaa chupi ya jina ataipandisha kidogo/atashusha suluali kidogo ili ionekane? Au kwani huoni pia mtu akisafiri na ndege huwa hatoi ile lebo/sticker ya kilos? atatumia begi/sanduku hivyo hivyo na ile sticker hadi apate safari nyingine ya ndege ndio aondoe ile iliyopo! leboozzzz juuuu

    ReplyDelete
  23. Hio suti hapo juu muulize michu anayo tokea lini na yeye hajatoa Lebo unafanya kitu ile roho na penda kama hobi yako unajisikia babu kubwa kuwa na lebo powa injoi tu hata Bekamu ana vaaa na lebo

    ReplyDelete
  24. ina maana tunatakiwa tutoe na alama zote za magari mfano toyota,suzuki nk?

    ReplyDelete
  25. Wadau wote msiojua maana ya lebo kuwekwa, hususan mkono wa kushoto mwa koti.
    Hii ni kumsaidia muuzaji na mnunuaji dukani kutambua ni brand name gani ya suti anayouza au kununua. Mara nyingi huwa zinapangwa katika safu za kuning'iniza madukani.
    Imeungwa na uzi hafifu ili iondolewe, unlike jeans where the whole label is doubly stitched on.

    Mifuko yote pia huwa imefungwa kwa uzi mwepesi, mnunuaji ni kazi yako kuutoa.

    Ushamba huu umekithiri mno, hasa kwa WATANZANIA, na Waarabu wa Yemen.
    Ni kati ya mijitu mishamba inayoongoza duniani!
    I can underand the Yemenis, as they hardly wear any western dress at all but for the Tanzanians, it's ushamba big time, pure and simple!
    Hebu tuacheni jamani..... mnatutia aibu..

    ReplyDelete
  26. Wewe Anonymous was Wed Jan 19, 02:50:00 PM 2011 uneathirika na brainwashing. Nadhani unajua TZ na Yemen tu. Tuliotoka sehemu tofauti tumeona watu wengi tu wakivaa suti na hizo lebo: Brazil nimeona, US nimeona, Mexico nimeona, UK nimeona na hata nchi nyingi tu za Europe. Hapa East Africa Kenya na Uganda ndio usiseme. Si TZ na Yeman tu. Hakuna offence yoyote kuacha hiyo lebo. Na mimi zangu sitoi!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...