
Angalizo la leo linahusu habari kuondoka haraka ukurasa wa kwanza. Hii ni kutokana na muongezeko wa spidi ya kuposti habari mbalimbali kwa siku, kiasi hata habari zingine hazikai muda mrefu ukurasa mkuu. Hii mdau isikutie hofu kwani hii imeshapatiwa ufumbuzi toka muonekano mpya uzinduliwe takriban mwezi mmoja uliopita. Yaani habari zilizopita hazipotei bali zinahifadhiwa katika sehemu maalumu ili wewe uweze kutembelea bila shida.
Ni kwamba endapo hutoona ama hototosheka na libeneke la ukurasa mkuu kwa siku husika, usisite kubofya katika 'Habari Zilizopita' chini kabisa upande wa kulia, nawe utapata ukitakacho. Kama hujapata bofya tena 'Habari Zilizopita' hadi ufike unakotaka. Kwa mdomo mwingine ni kwamba hakuna habari ama taswira iliyopita utakayokosa kuiona endapo kama utabofya 'Habari Zilizopita.' Vile vile spidi ya Globu ya Jamii imeongezwa maradufu hivyo kwikwi hakuna tena. Yaani ukigusa tu ngoma inafunguka bila shida. Yote!
Vile Vile chukua muda kudadisi na kupereruzi katika 'KUMBUKUMBU' pale juu kulia, chini ya picha ya Ankal, ambapo libeneke la kila mwaka tokea mwaka 2005 hadi leo limewekwa bayana. Na sio mwaka tu bali kila mwezi wa miaka hiyo mitano iliyopita ipo kwa ajili yako. Usisahau kwamba utapobofya 'Habari Zilizopita' katika mwezi unaoperuzi, ujue utarejeshwa nyuma katika mwezi husika hadi mwisho wake. Yaani hapa hakuna kulala!
Vile vile ukiangalia juu ya picha ya Ankal pale juu kulia, utakuta kuna nembo za Facebook, Twitter na Youtube. Hivyo vyote ni vipiga chapuo vya Globu ya Jamii ambapo utakutana na Ankal katika hizo Social Media na utaruhusiwa kudadisi na kuperuzi bila kelele wala mikwaruzo. Video kibao utapata, twits za nguvu utaziona na stori katika Facebook utazikuta kibao.
Kwa mdau mwenye swali, ushauri ama hata mkosoo andika email yake kupitia issamichuzi@gmail.com nawe utasikilizwa na kujibiwa chap chap.
Karibu sana mdau ufaidi uhondo wa
Globu ya Jamii.
-MICHUZI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...