Habari Wadau wa Tasnia ya Filamu nchini.
Karibuni katika warsha ya kuzungumzia filamu za Kitanzania....
ni Bure kwa kila mtu.
Karibuni wote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. itakuwa vyema sana kama kina kanumba na mwenzake ray na wengine wapate nafasi ya kujifunza na wataweza kuacha kutengeneza soap opeara na maigizo na wacheze sinema zinazolingana na hali yao na zenye authenticity

    ReplyDelete
  2. Duh wabongo mna akili. Nimerudi nyumbani juzi tu na nilinunua movie 30 (lakini ni 15) kwa vile kuna part one and two kwenye kila movie. Nimeangalia chache bado sijamaliza ila kila ninayoangalia nishindwa kukata kiu ya kusema nimeona movie. Nilikua najaribu nielewe ni nini hiki? Sasa umenipa jibu hapo juu hii ni soap opera kabisa. Hizi hamna hata moja ambayo ni movie kweli ninayoangalia mpaka sasa hivi.

    Huko mnakokutana naomba muwaambie
    1. Wasipige makelele wakati wanaongea kama wanigeria..

    2. Edit out sehemu zisizo muhimu. part 1 and 2 haina umuhimu kabisa ni kupoteza muda wa watu. Mnacheza scene moja dakika 10 bila sababu yeyote..Kama ni hela muuze basi mbei ya juu zaidi iwe part moja tu.

    3.Msichanganye kiswahili na kingereza. kama wote mwaongea kiswahili basi iwe kiswahili kama ni kidhungu basi wote muongee kidhungu..

    4. Wasiige kubeba fimbo kama wa nigeria be authentic.

    Ni hayo tu lakini mtafika tu ukisikiliza ushauri wa wateja wenu mtafika mbali sana.

    ReplyDelete
  3. Ushauri wangu ni,muache kuonyesha kipande kimoja au kuwa sehemu moja kwa muda mrefu.Lile onyo linalotolewa na yule bwana Mkinga wa Cosota, la kutonakili au kuonyesha sinema ktk.vibanda nk.liondolewe, kama ni warning itolewe kwa maandishi tu kama cinema zinginme za hollywood nk.Kuweka jisura la mtu akitoa onyo
    kama vile yeye ndiye msanii sio vizuri,mtu kama huyu huo wadhifa alionao ni wa muda tu je? akibadilishwa kikazi itakuwaje??
    pia hii inampa mwanya wa kupokea rushwa au kushirikiana na hao hao mahasidi wanaoiba kazi zenu za kisanii.Pia sioni haja ya kuonyesha ile "behind carten"kwani haina maana yoyote.Najua kuiga siyo vizuri ila natoa ushauri jaribuni sana kuiga mifano mizuri ya cinema za hollywood,kwani wao wana experience ya miaka mingi na pia wana mafanikio makubwa.Jingine ni wacheza cinema wetu mnajitahidi sana kujiendeleza ikibidi ki masomo
    hasa mambo yahusuyo uigizaji wa filamu ili muweze angalau kufikia kwenye level ya kimataifa.msiridhike na kiwango mlichonacho.Jaribuni kujiepusha na kashfa za kila siku tuzionazo kwenye magazeti maana zinatuchefua sana,mizunguko ya kwenye mabaa,kashfa za ngono,ulevi,ugomvi kila siku pia punguzeni ili kujenga heshima ya profession yenu.
    natoa maoni haya kwa kuwa mimi ni mpenda sinema za kiswahili na huwa nafuatilia sana mambo ya sinema za huko nyumbani Tz.
    mdau Dallas,Tx.Usa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...