Brother Michuzi,

Habari zako, heri ya mwaka mpya. Naomba uniwekee swala langu hili katika blog yetu ya jamii ili wadau waweze kujadili na kunielimisha juu ya hili lilinonisibu. samahani stori ni ndefu kidogo.

Katika sherehe za mwisho wa mwaka, kuna Mtanzania mwenzetu hapa UK alifanya tafrija na kualika watu kam 30 hivi kutoka nchi mbali mbali kutoka Tanzania na nchi nyengine mbali mbali. Mimi nilikuwa mmoja wao. Katika tafrija hiyo takriban watu wote ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kukutana nao. Wote walikuwa ni wapiga boksi (kama tunavyoitwa na wenzetu waliopo nyumbani) wenye professional zao za uhakika.

Katika kujtambulisha na kuweza kuwa na mazungumzo, majadiliano mengi mwanzo yalianzia kama "umemjulia wapi mwenyeji wetu?" "unafanya kazi gani?" "unafanya kazi wapi?" n.k. Katika maongezi hayo niligundua kuwa kuna watu ambao professional zetu ni moja na pia wale ambao walikuwa na mawazo na idea zilizonipendeza na nilipenda kama nitaweza kuwa na contact nao zaidi baada ya sherehe. Kwa wengi hii ilikuwa chance nzuri ya ku-expand my network. Kwa sababu hiyo nilibadilishana business cards na baadhi ya wageni wenzangu na pia kuchukuwa number za simu na email address kwa wale ambao hawakuwa na business cards zao.

Cha kushangaza sana ni kuwa nilipojaribu kupata contact za dada mmoja wa kitanzania, alinijibu kuwa yeye ameolewa na hayuko interest na mimi, jambo ambalo liloinifanya nijitetee kwa nguvu kuwa hilo sio lengo langu langu, lengu langu ni ku-keep intouch naye kwa vile sote tunatoka tanzania, sote tuna professional sawa na nilipenda maoni yake juu ya Tanzania. Hapo alirudi matawi ya chini na ingawa sikutaka tena details zake atleast nilimpa business card yangu.

Pia nilipoondoka katika sherehe na kabla hata sijafika nyumbani kwangu, nilipata texts 3 katika mobile yangu kutoka kwa akina dada watatu wakitanzania niliokutana nao katika sherehe, wote wakiniambia kuwa nisiwasiliane nao kwani wamegunduwa mchezo wangu. Text zote zilikuwa na maneno sawa sawa, jambo ambalo lilinifanya nimpigie simu mwenyeji wetu wa sherehe nilipofika nyumbani kwangu, na kutaka kujua kilichosibu nilipoondoka katika sherehe.

Nilichojulishwa ni kuwa baada ya kuondoka akina dada wale watatu katika kuzungumza zungumza mmoja alisema kuwa nimechukuwa number yanke ya simu na alikuwa so excited lakini mood ilibadilika pale alipogundua kuwa sio peke yake ambae nimechukua number yake ya simu. Kwa ufahamu wao wote watatu ni kwa vile nimetaka contact zao basi nilikuwa naashiria kuwa niko interested nao na kwa wao kuwa walinipa ni kwa sababu walikuwa wako interested nami na walikuwa wanategemea kuwa nitawasiliana nao and see whats gonna happen next! Hili lilinishangaza sana hususan kwa vile mwana dada mwengine wa mwanzo alivyonijibu nilivyotaka contact zake. Ilibidi nimueleze mwenyeji wetu nilichofanya na kuwa nimetowa card zangu kwa watu zaidi ya kumi na mbili wanaume na wanawake na lengo langu ni ku-expand networking na sio mengine, mwenyeji wangu alicheka na kusema "wabongo wanatafsiri vyengine ukiomba number za simu" jee hili ni kweli

Ninachotaka kujua ni kwa nini watanzania wakiombwa number za simu wanahisi kuwa unawataka? Kama ni hivyo mtu afanyeje ili aweze kupata contact za mtanzania bila ya kudhaniwa kuwa una make a move?.

Ahsante sana
MDAU T wa UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Pole sana mdau, hayo ndiyo mambo ya kibongo bongo.Ni kweli wakati mwingine hata mtu unaona kero kwenda kwenye mikusanyiko ya kibongo kwani unakuta baadhi ya wabongo ( sio wote ) wana vijitabia vya ajabu; ikiwa ni pamoja na kumzungumza mtu vibaya tabia ambayo wenzetu wa nchi za magharibi hawana.Kuchukua contacts za mtu tofauti na mbongo baada ya mazungumzo ya kufahamiana ukizingatia kuwa wote mna taaluma na kazi zenu;si tatizo hata siku moja; na tena wanasisitiza kuwa mtafutane ili kupanua mtandao wa kufahamiana - (Network). Ila sisi wabongo nadhani baadhi yetu mambo ya kiswahili swahili bado yametukaa; hata kama mtu ameelimika na kujua maana ya kuwa na mtandao wa marafiki ni nini. Baadhi wanaishia kuwa watu wa majungu tu;nadhani ni tabia za wachache tu.Ila pia kuna wabongo ambao wana tabia za namna hiyo; wanachukua nafasi kama hizo ili kujiepulia akina dada; na watu kuchukua tahadhari ni jambo la kawaida.Tatizo linakuja hapa kuwa walizungumzia swala la wewe kuchukua contacts, na kujikuta kuwa wote wametoa contacts; hivyo wakadhani wanachanganywa; ila ni ufinyu wa mawazo kuanza kufikiria kuwa kila anayechukua contacts zako anakutaka;unajuaje kuwa ndiye atakayekusaidia katika jambo fulani wakati fulani?
    Wabongo; popote;ughaibni; nyumbani; tuamke.Muda wa kupiga piga majungu haupo.Muda wa kuzungumzia fulani hivi;fulani vile;haupo; ingia kwenye mtandao fanya utafiti;soma magazeti;nk;kuliko kukaa na kupiga majungu.Huku kukaa bure ndiko kunakosababisha hayo;fulani alinipigia simu baada ya sherehe;nk nk nk.Huo ni muda mchafu. Kujirekebisha ni muhimu; swala la kuwa na contacts za mtu ambaye amekuwa inspired naye kitaaluma au kikazi; au hata kimaongezi ni swala la kawaida.
    Tuamke.Tuamke.
    Pole mdau.
    Next time umepata fundisho; akina dada - approach with care; chukua contacts mkiwa in a group.
    Kila la heri

    ReplyDelete
  2. Pole sana Bro! ni kweli huku bongo ndio hivyo, na umenikuna kabisa, huwa nakerwa sana na tabia hii. Stori yako kama vile nilikuwepo, yaani baada ya hao wadada kuona unachukua contact kwa dada zaidi ya mmoja wakajua unataka kuwachanganya na si ajabu aliyekuambia ye ameolewa ungeanzia kwake angekupatia contact zake, si ajabu pamoja na kuwa wana professional zao lkn wako huko kwa biashara za 'uchunaji'

    WATANZANIA FIKIRA ZETU ZIMELEMEA PANDE MOJA TU hasa kwa wenzetu walio kimbia umande! cha kushangaza hataambao hawakukimbia umande nao pia bado wana kasumba hiyo hiyo.

    ReplyDelete
  3. Mara nyingi ukiomba namba ya mtu hususani kwenye tafrija, ni kwamba ungependa mjuane zaidi. Mara nyingi huwa ni kutaka kuanzisha mahusihano. Lakini hii ni juu ya tafsiri na jinsi ulivyoomba namba. Ni vizuri ukasema mwanzoni kuwa unaomba namba kwa madhumuni gani hususan kama ni akina dada wa umri wako. Ila kusema ukweli, kwa jinsi ulivyojieleza, ningewalaumu wao sana sana kwa kufikiria mbele sana.

    ReplyDelete
  4. Mimi ni mwanaume kama wewe lakini ukweli wenyewe unategemea umeomba namba ya simu katika mazingira gani. Hata hapa nilipo (USA) ukimwomba dada yeyote namba ya simu atakuuliza why do you want my number or my boyfriend won't like that. Pia itategemea na wasifu wako wa nje wewe muombaji wa namba, inabidi tuelewe kuwa wakina dada au mama wote wameumbwa hivyo cha msingi kabla ya kuwaomba namba lazima uwaeleze sababu ya kimsingi wakuelewe. Hata wewe mwenyewe uwezi tu mke wako au mpenzi wako akawa anatoa namba tu kwa watu ukashangila kitendo hicho.

    ReplyDelete
  5. MJADALA WA LEO: HIVI KUMCHANGIA MTU KWENYE HARUSI NI LAZIMA?

    Ndugu Michuzi, pole na majukumu ya kijamii.
    Mimi naomba uweke hii hoja kwenye blog ya jamii ili wadau watoe maoni yao.
    Swali la kizushi ni hilo hapo; kwani ni lazima kumchangia mtu kwenye harusi?
    Natambua kuwa kama wajibu wangu kwa jamii;maswala ya kujumuishana kwenye shughuli ni ya kawaida, na huwa najali sana hilo. Ikiwa una majukumu mengine yanayokuzuia ukashindwa kushiriki kwenye michango ya harusi;je; mhusika ana sababu ya kuanza kupayukapayuka mitaani kuwa fulani hakunichangia?Huu ni ustaarabu?
    Mbona kuna ustaarabu mwingine wa mtu anatoa mchango wake wa (support) baada ya harusi ili maharusi wawe na nyongeza kidogo ya kuanzia baada ya kukaukiwa mifukoni kipindi cha maandalizi?

    Naomba wenzetu mnaoishi ughaibuni mniambie nyie huko mnafanyaje, mnachangiaje harusi? Changa nikuchangie au? Hebu wadau mtoe maoni yenu hapa.

    Mdau Morogoro; Mji Kasoro Bahari

    ReplyDelete
  6. Tatizo ni Elimu Dunia. Naku feel bother wala lisikuchanganye. Hawa dada zetu wa kibongo wanamchecheto na masuala ya relation kwani umri unakata na makaratasi vilevile yanawasumbua kichwa.

    ReplyDelete
  7. pole sana mzee,asilimia kubwa ya dada zetu hapa UK ndio walivyo,kunguru hata umsafishe vipi ka tabia hakaishi.dada wa ki Nigeia au wa Congo unaongea biashara kama mwanaume tu,siku nyingine uwe carefull na useless hao.

    ReplyDelete
  8. Acha zako bwana wamekufuma unaleta usomi hapa!
    mtu humjui unataka kumuuliza kuhusu tanzania wee huijui au vp?!
    na wanaume ndo nyinyi wa kibongo mwanamme gani wa kibongo yuko tayari kuona mkewe anapigiwa cm na wanaume ovyo kisa mmekutana kwenye party si atakufumua siku hiyo hiyo?!
    anza wewe kwa my girl friend wako au my wife wako kumruhusu kutoa toa namba yake ovyo kwa wanaume halafu akianza kupigiwa ndo utapata jibu why!

    ReplyDelete
  9. kwanza nakupa pole sana kwa yaliyokukuta kaka,nami pia nipo nje ya nyumbani hapa UK na hilo unalolizungumza ni kweli lipo kwani hata mimi limewahi nikuta ktk mazingira yanayofanana na hayo,Na kwa mtazamo wangu huo ni ufinyu wa mawazo na upeo wa kufikiria lakini pia kujifanya wanajua eti tu kwasababu wapo ulaya.Heshima na utu daima ni vitu vya bure kabisa.....ushauri wa bure kwa dada zangu hebu acheni kujifanya mwajua wakati mwaungua jua,maisha haya mafupi sana hatuna budi kupendana na kusaidiana na siyo kuhisiana vibaya.
    Na wewe mdau uliotoa comment za kufumaniwa nana ni walewale kama siyo mmoja ya waliofanya tukio hili na kama ndiye basi badilika......

    ReplyDelete
  10. Pole kwa yaliyokuta. Sijui kama unalijua hili lakini tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wana-network tofauti na wanaume. Wanawake huwa wanapenda kutengeneza mahusiano zaidi na pia kusaidiana. Wanawake wanapenda zaidi kufanya business na watu wanaowafahamu tayari. Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa kuwa mwanamke ata-network na mtu fulani baada ya kupata referenece/referral toka kwa mtu anayemwamini. To women, it's all about connection and trust.

    Kwa sisi wanaume tuna-focus zaidi kwenye business. Tunamind zaidi biashara kuliko friendships. Inawezekana labda baada ya wewe kuondoka walipata reference kuhusu wewe toka kwa mtu wanayemwani? Just asking.

    Tovuti ya Forbes ina article nzuri sana on “Understanding How Women Network”. Inapatikana hapa: http://www.forbes.com/2009/10/07/networking-relationships-connections-forbes-women-entrepreneurs-men.html

    Pili, tujaribu kutofautisha kati ya “networking” na “socialising”. Inawezekana kabisa kuwa wakati wewe ulikuwa pale ku-network, wao walikuwa pale ku-socialise. Labda tujiulize ni wangapi wangehudhuria kama wangealikwa kwenye networking event inayohusiana na fani/interests zao?

    Tatu, pia inabidi tutofautishe kati ya ku-network au kuji-promote. Ni rahisi kwa networker kuji-promote bila kijijua. Nimeshughudia mara nyingi tuu kwenye networking events ambapo watu walikuwa wanajipromote zaidi badala ya ku-network. Kuna tofauti kubwa sana hapo. Na hapa ndipo linapokuja suala zima la “networking skills”.

    Nne, networkers waliobobea wanashauri badala ya kuomba namba za simu za mkononi, omba email addresses.

    Mwisho, hili lisikukatishe tamaa kwenye shughuli zako za ku-network. It just shows that men and women are different especially when it comes to networking. Women and men tend to think differently in many ways and have different traits so we have to accept these differences. So, next time when you are at a female networking event or a mixed one just be yourself but accept our differences.

    ReplyDelete
  11. anonymous wa Jan 11:42:00 pm 2011, wake up and smell coffee, uko ulimwengu gani? networking ni muhimu sana katika pirika za kikazi, sio kila anaekupa business card yake na kutaka contact yako ndio anataka kukupeleka kitandani. Sio kila mtu akili zao ziko katika maingiliano kila dakika. Amka na uwache ushamba wako, mkeo au girlfriend wako kuwa na number za mwanamme mwengine haimaanishi kuwa wana affair.

    ReplyDelete
  12. Siamini kuwa wachache wamekuja hapa na mentality ile ile ambayo mleta mada imemkuta. Watanzania tutaamka lini na kuacha kufikiria kila kitu ni ku@@@bana? Watu wanabadilishana business card kila siku na ni jambo la kawaida dunia nzima lakini watanzania bado tunaona mtu akiombwa number ni kwa sababu unataka kulala nae tu!

    ReplyDelete
  13. miye ni mwanamke naelewa ukiwa nchi hizi za watu utapenda kujuana na watanzania wenzako maana hao ndio ndugu zako.
    kwangu mimi nauliza
    1.. ulivyowaomba hao dada cmu zao kwani mliongea nini hadi wote wakutext maana hapo inaelekea kuna kitu ulisema .
    2.kwa hao wadada nadhani kila mmoja alikuchukuliwa vingine (labda mawazo yao finyo kuwa jamaa ananitaka)hapo ndio shida zetu mwanamke ukimwomba # yeye amefika mwisho jamaa ananitaka ambako saa nyingine sio.
    Kwa upande wangu mimi nitakupa # yangu na nitakuambia my status right away maana nataka tuwe kwenye line moja sio kesho uniambie mbona ujaniambia na nitakuambia mda mzuri wa kunipigia maana tupo busy all the time.

    Pole sana kaka ni communcation zero na sio tu wanawake wapo hivyo hata wanaume utamwambia # yako ngapi kesho utasikia demu ameniomba # yupo desperate kwa hiyo tusilaumiane upande mmoja pande zote tunamatatizo.

    Bibie USA

    ReplyDelete
  14. Jambo la kawaida kabisa watu tunapokutana wa kutoka nchi moja ni ndugu, na ni faraja kubahatika kukutana na ni nafasi ya kutambuana na kuachiana njia za mawasiliano. Nimeishi nje ya Tanzania na nimeshuhudia uliyosema hasa Europe na Marekani.

    Kwa uzoefu wangu angalia watu unaobadilishana njia za mawasiliano, hasa kiwango cha elimu na kama wako stable. Wengi wasio stable ni matatizo tupu kama alivyosema mmoja hapo juu. Niliwahi hudhuria sherehe moja kama hiyo Jijini NY ikawa mwanzo na mwisho toka hapo tukaamua watu wenye profesheni zetu na tuliotulia kuwa na mikusanyiko yetu, kwani vinginevyo ni majungu, vijembe, vishoka, dharau, na mengineyo. Ukiwa mstaarabu mno wanakuona kama unaringa kuliko mwanamke. Ukijiachia kuongea na kila mmoja unaonekana mtafutaji. Ukiwa mpenda kujadili maendeleo wanakuona we unawadharau au kuwadhalilisha na kwamba umeshaondokana na umaskini.

    Jamani wabongo tubadilike.

    ReplyDelete
  15. Mtu yeyote awe mwanamke au mwanaume awezi kupatia namba mpa ajue lengho lako ni nini????? msitake kujifanya eti tumekaa nje ya tanzania basi wanawake wa kitanzania ni washamba, sio hivyo kumpampa mtu namba mpaka umjue vizuri hata kama mmekutana siku hiyo inabidi umueleze who you are then afanye maamuzi!!

    ReplyDelete
  16. Mimi ni mwanamke na naongea kama mwanamke. Sio kila gathering watu wanatoa toa number zao tu. Wanaume wengi wa kibongo nao wana mchezo huo wa kuomba number za simu za kila msichana kwenye mahali popote wanapokutana. Kama umeongea na mwanamke na hata kama field zenu ni moja mwingine hataki kuwasiliana na wewe kwa vile unaweza ukawa wewe sio mtu ambaye angesocilise na wewe au hata kukeep contact na wewe nje ya hapo kwenye hiyo sehemu mliokutana. Wewe kuwa na kazi sawa au kisomo sawa na mimi sio sababu ya mimi kuwa na contact zako. Wewe girl friend wako, mchumba au mke wako akitoka kwenye party akaja na manumber ya watu kibao utajifikiria vipi? Sio kuwalaumu wanawake wa hapo UK tu kwa sababu zenu na kuwaita kunguru. Kwani nani anawaharibu hao wanawake si nyie nyie? sijui tuwaite mqwewe..

    Nakushangaa ulikwenda kwenye party au ulikwenda kutafuta contacts. uliacha kadi yako kwa watu kumi na mbili kwenye party moja? I am sure ulikua na lako na wamekushtukia. Nikienda kwenye party nikakutana na mtu labda tuwe tumeongea kwa saa moja au zaidi ndio nitatoa number yangu na nimuone ana personality kama yangu. Just hey hey bam this is my number..Wao ulikua kwenye speed dating nini?

    ReplyDelete
  17. noma iyoo nduguu yangu

    ReplyDelete
  18. Kwani ni lazima watu wakupenamba zao?
    Wakisema hapanamaana yake ni hapana na hauna sababu ya kuwaulizani kwa nini wamekukatalia.
    Huu ndo tunaita mfumo dume,watu wasikatae kukupa namba zao uwasemesemetuu. Mimi nawapongeza walokukatalia kwa kuwa unaonekana kabisa kuwa ufahamu wako ni mdogo.

    Kutoa contacts zako kwa mtu ni kuwa unakubali kuwasiliana na kuanzisha uhusiano naye. Sasa si kila mtu anataka kuwa na uhusiano au mawasiliano na wewe,hilo ulijue, ukikataliwa usiite watu washambna, wewendiye mshamba, unadhani kwa kuwa unjiita kuwa na kazi nzuri basi kila mtu akushobokee, NOOOOOOO!!!!!

    Grow up bro!!

    ReplyDelete
  19. Pole sana Mdau... Mimi ninavyoelewa, ukiwa nje ya nchi unakuwa huna ndugu, na mtu yeyote wa kutoka nyumbani (nchini kwako) unamthamini kama ndugu, kuna leo na kesho, shida na matatizo yapo kwa kila mtu, nini maana ya jamii ya watu wa nchi fulani mahala fulani... hao wadada wana corrupt minds, wanajali ngono kuliko undugu. Wapotezee

    ReplyDelete
  20. mawazo finyu na mgando, ndo maana hatuendelei....

    ReplyDelete
  21. Kaka!
    Usipate tabu, maana fikra za watu ziko tofauti. Mimi imenitokea sana hata nimenyimwa numba hata pengine kudharaulika.

    Well hainiumi sana kwani huwa naamini ktk mimi na nia yangu mtu akifikiria vitu vingine yeye ndo ana mawazo hayo.

    Nawe kuwa kimya, na nadhani ukubali hao si watu wa aina yako.

    Asante.

    ReplyDelete
  22. Tumetofautiana sana mitazamo so kabla hujaomba or kugawa namba hakikisha unaona mtu huyo mnauelewa unaoendana otherwise matatatizo

    ReplyDelete
  23. Ohoo kaka unaishi mji wa Reading au Milton Keynes nini? Au pengine London? Huko hakuna tofauti na Bongo mambo yote ya umbea na udaku yanapatikana ndio maana walikujadili ulipoomba namba za simu. Sioni kwanini iwe ni big deal hao walioombwa namba za simu au contact zao si wangesubiri kinachofuata? Walikuwa na kiherehere gani cha kuanza kuambizana kuwa so & so kaniomba namba? Hapo ujue ulivyoondoka tu umegeuka topic kwa Watz hawajui wala hawaoni opportunity ya kufanya mambo ya maana zaidi ya kuwaza relationship, si wanaume wala wanawake. Kwa sababu mimi ni mwanamke na najua yangetokea yale yale kama ningeomba mimi hiyo namba.

    Ushauri wa bure;
    Unawajua Watz kibao lakini huwajui watu wa mataifa mengine, why dont you network with them? Maana ulipokuwa Tz ulikuwa umezungukwa nao sasa huku ughaibuni ndio wakati mzuri wa kupanua netwok yako na kujuana na watu wa mataifa mengine. Hii mambo ya kujidai ooh nilitaka kujuana na Watz wenzangu kwani huwajui? Si vyama vya Watz vipo, iunge huko utakutana nao kwenye sikukuu za kitaifa au jiunge na tawi la ccm/cuf utawakuta wanachama wenzio huko otherwise usitafute kusutwa bure maananeno ukimwambia mmoja litafika maili moja na maan tofauti. au tumia facebok kunetwork!

    ReplyDelete
  24. Lugha Ina-matterJanuary 11, 2011

    Mpiga box jitahidi basi kunyosha kiingereza chako.

    Kuna tofauti kati ya neno "Profession" (ambayo ni noun) na "Professional" (ambayo ni adjective)

    Na hii sio kwako tu, ila kuna sehemu zingine nimesoma kwenye hii globu na kwenye forum zingine za watanzania watu wanachanganya sana haya maneno.

    Chungulia dictionary utapata maana za haya maneno mawili. Na baadhi ya matumizi ni kama ifuatavyo (nitachukua mifano hai toka kwa mpiga box aliyetuletea maada:


    WRONG: Wote walikuwa ni wapiga boksi (kama tunavyoitwa na wenzetu waliopo nyumbani) wenye professional zao za uhakika.

    SAHIHI: Wote walikuwa ni wapiga boksi (kama tunavyoitwa na wenzetu waliopo nyumbani) wenye profession zao za uhakika.

    WRONG: Professional zetu/zao
    SAHIHI: Profession zetu/zao

    Mifano mingine ni kama vile:

    SAHIHI: I am a professional
    SAHIHI: My profession is ....

    WRONG: Tuheshimu professional za watu.
    SAHIHI: Tuheshimu profession za watu.

    Samahani kwa niliowaboa (wale wasiopenda marekebisho ya lugha kwa kudai kuwa mradi wameeleweka).

    Lakini ni vizuri kuweka jitihada ya kuongea lugha fasaha kila inapowezekana, maana kwa watu makini wakishasikia lugha yako sio fasaha hawakusilizi tena wanaassume kuwa huna upeo wa kutosha kujenga hoja makini.

    ReplyDelete
  25. Wewe kaka umeandika humu kujiosha. Kama umetokea Bongo basi unafahamu fika kuwa ukiomba namba ya opposite gender inamanisha upo interested nao. Wabongo kokote bana, hata huko tabia zao hazibadiliki. Kama unataka mambo ya kidhungu ungeomba namba za wakware vinginevyo afadhali ungechukua email! Loh

    ReplyDelete
  26. Kaka.. pole sana ila wakati mwingine inabidi ukubali hisia za watu. Unajua kila binadamu anaprincipal zake za maisha na siyo lazima ziwe na jinsi unavyotaka wewe. Pengine hao wadada they dont want anything from you ndiyo maana wakaona siyo lazima wakupe number zao....Lakini mungu mkubwa wanaweza kukuona ni mtu wa thamani sana once they got a big problem and you become a survior to them... kwa mfano, wamefukuzwa kwenye nyumba alafu wewe ukawapa accomodation kwa muda au wamekamatwa ukawawekea udhamini.....

    ReplyDelete
  27. Wewe bro acha hizo bwana. Nawashangaa sana hawa waliokupa pole haba. Usitake kutufanya sie watoto na kuwachafulia jina dada zetu walioko huko. Wewe kadi kumi na mbili unatoa kwenye sherehe ya watu 30 wapi bwana wewe. Wewe hao dada uliwapa/uliwaomba namba kwa misingi ipi? Katika hayo maongezi, je ulikuwa muwazi kuhusu nia yako ya kuomba/kuwapa namba yako? Wote tunaelewa umuhimu wa networking. Usitufanye sie watoto. Wewe kama uliwaambia hao kina dada kwa uwazi kabisa kwamba ungependa kuwasiliana nao kwa sababu ya ajira na elimu zao sidhani kama wangekutumia hizo texts masaa kadhaa tu baada ya hiyo sherehe kuisha. Mawasiliano kwa ajili ya networking mara nyingi huanza at least the next day and usually to show gratitude for meeting them and hoping to continue communication. Wewe umelikoroga ukaona ukimbilie michuzi blog uje ujioshe mikono baada ya hao kina dada kukushushua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...