JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ofisi ya Bunge inapenda kuwatangazia Waheshimiwa Wabunge wote kuwa kutakuwa na mafunzo ya awali (Orientation Course) yatakayotolewa kwao kuanzia tarehe 25 Januari, 2011 mpaka tarehe 3 Februari, 2011.

Mafunzo hayo yatatanguliwa na vikao rasmi vya Vyama vya Siasa kikiwemo CCM ambacho kitakuwa na semina kuanzia tarehe 22 – 24 Januari, 2011. Kikao cha Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitafanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Kwa taarifa hii, Waheshimiwa Wabunge wanaombwa kuwasili Dar es Salaam kwa kuzingatia tarehe ya vikao hivyo vya mafunzo.

Eliakim P. M. Mrema

KAIMU KATIBU WA BUNGE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Sasa wewe umekuwa KATIBU wa CCM. Kwanini mnajigonga kwao. Basi tupe na ratiba ya CUF, CDM, TLP, NCCR-MAgeuzi, UDP

    ReplyDelete
  2. waheshimiwa wabunge wawasili dar-es-salaam...?? kwani kwa sasa wanakaa wapi..?? wao siku zote wanakaa dar, maybe kikao kingekua dodoma hapo sawa...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...