Bw. Abdallah Mohamed Zombe

HATIMAYE aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Mohamed Zombe, ametangaza rasmi nia yake ya kuishitaki serikali kwa hoja kuwa ilikiuka sheria na Katiba ya nchi wakati ilipomkamata na kumfungulia kesi ya mauaji.

Zombe alikamatwa mwaka 2006 na kufunguliwa kesi ya mauaji ya watu wanne lakini aliishinda serikali katika kesi hiyo.

Uamuzi huo ameutangaza baada ya siku 90 alizotoa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumwomba radhi na kumlipa fidia ya sh bilioni tano kumalizika.

Habari Kamili tembelea Tanzania daima;

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hili linaonekana kama mzaha lakini laweza kuwa Dowans nyingine si mnajua Tanzania Shamba la bibi

    ReplyDelete
  2. nini? eti alipwe fidia billion 5?

    ReplyDelete
  3. hii ndo Tanzania y sasa bana,, full ze comedy!!!!!

    ReplyDelete
  4. Eheeeeeeeeeeeeeee Mwananzengo Mabilioni tano yote..Weeeee acha bwana hiyo mbona walipa kodi kutakamliwa mpaka dmu sasa mara IPTL,DOWANS..Mara wa EPA..MMMMH,mara wastafu aw Afrika mashariki..

    BASI BWANA NAONA TUUZE NCHI TUGAWANE KILA MTU CHAKE...

    MZEEE WA BK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...