Baadhi ya visura wataoshindania taji la Kisura wa
Tanzania wakiwa Kiromo View Resort huko Bagamoyo leo
Kisura Kipuyonde Laiboni kutoka Monduli akiwa na mchumba wake bwana Paulo katika hoteli ya Kiromo View Resort, Bagamoyo, mkoa wa Pwani ambako kambi ya Kisura wa Tanzania imeanza rasmi leo. Mrembo huyu ameingia kambini akiwa na mchumba wake huyo na kaka yake ambao wamekuja toka Monduli kuona kama kuna usalama ama la...
Kisura wetu akiwa na kaka yake Mshangamal Laiboni.
Kisura akiwa na kaka na mchumba wake huko Bagamoyo, leo

Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. I don't think it's a good idea to pluck someone straight out of that environment and throw them into a completely new/strange/foreign one such as this one. I feel bad for the poor girl. She looks completely out of place. Praying she can handle all this pressure. Best of luck.

    ReplyDelete
  2. kama flaviana

    ReplyDelete
  3. Mashindano ya urembo yamekuwepo katika tamaduni zote hapa duniani. Kila utamaduni umekuwa na vigezo vyake na namna yake ya kupima urembo. Makabila yetu nayo yana jadi hizo huko tulikotoka. Wale waliosoma kitabu cha Okot p'Bitek kiitwacho "Song of Lawino," wataelewa kirahisi ninachosema.

    Dada huyu wa ki-Masai anatufundisha mambo ya msingi. Analeta changamoto nzito kwa kuja akiwakilisha urembo wa ki-Masai. Kwa mtazamo wangu, fundisho hapa ni kwamba tunapaswa kujitambua asili yetu. Kama ni mashindano ya urembo, tutumie vigezo vya kwetu, si vya kuiga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...