Sheikh mkuu wa Tanzania, Sheikh issa Bin Shabani Simba, akiwahutubia waumini wa dini ya kiislam na wadau wa elimu, waliohudhuria harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana na bwalo la kulia chakula katika shule ya sekondari Geita Islamic Seminary, wa tatu (shoto) ni mkuu wa wilaya ya Geita ndugu Mh. Philemoni Shelutete.
Baadhi ya wana madrasa katika harambee hio
Viongozi wa dini ya kiislam waliohudhuria harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wasichana na Bwalo la chakula katika shule ya sekondari kiislam ya Geita kutoka kushoto wa tatu ni sheikh wa mkoa wa Mwanza Sheikh Salum fereji.
Wadau waliohudhuria harambee hiyo
Wadau wa elimu waliohudhuria harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana na bwalo la chakula la shule ya sekondari ya kiislam Geita. harambee hiyo ilifanyika hapahapa wilayani Geita, amabo sasa ni Mkoa.

*Muft Simba, aongoza harambee Geita, achangia milioni tano taslim.
*Asema matokeo mabovu ya kidato cha nne yamesababishwa kwa kuajiri bora walimu na si walimu bora.
*Jumla ya milioni 17,321,300 zilikusanywa.

Picha zote na khabari
na Shabani Simba wa Globu ya Jamii, akiwa Geita.


Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Bin Shabani Simba, amewataka waislam kuchangamka kuwekeza katika masuala ya elimu kwani elimu ndio mkombozi ma madhila yote yanayowakumba hapa nchini.
Na badala yake amewataka waislam waache kulalama na badala yake kupambana na vikwazo vyote vinavyowakabili.

Sheikh Simba, aliyasema hayo mjini hapa wakati akiendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wasichana na bwalo la chakula kwenye shule ya sekondari ya kiislam Geita. Katika harambee hiyo sheikh Simba alichangia kiasi cha shilingi milioni tano, fedha taslim.

Sheikh Simba, aliwapongeza waislam wa wilaya ya Geita na vitongoji vyake kwa kujikamua kujenga shule ya sekondari kwa nguvu zao. Lakini aliwaasa viongozi wa shule hiyo kutafuta walimu bora na si bora walimu.

Alisema madhara ya kutafuta bora walimu kutufundishia watoto zetu matokeo yake ndio haya ya kupata matokeo mabovu ya kidato cha nne ya mwaka 2010.Alisema hivi juzi juzi matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana yametoka na kiwango cha ufaulu kiko chini hali hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuajiri bora walimu na si walimu bora.

Aliongeza uwezi kuwapata walimu wazuri kama huna mshahara wa kutosha unaokidhi magumu ya maisha ya sasa hivyo aliwataka viongozi wa shule hiyo kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ili kupata fedha na hatimae kulipa mishahara minono itakayowafanya walimu wao wafikirie kazi yao tu ya kufundisha.

“Walimu hawasafiki nia kama hawajakirimiwa, maana yake walimu hawawezi kutufundishia vijana wetu kama hatuwajali” alisema sheikh Simba.

Aliongeza katika dini ya kiislam ukiwa na elimu ndio unakita katika uislam lakini kinyume chake ukiwa hauna elimu unakuwa kama kifaranga cha kuku anayeweza kupitiwa na mwewe wakati wowote.

“kama una elimu utakuwa unasikiliza la kila mtu bila ya kulichuAja kama linafaa au halifai na matokeo yake unayumba na kukosa msimamao muislam hatakiwi kuwa hivyo” alisema Sheikh Simbamba.
Aliwataka waislam kujitolea mali zao kwani kutoa ni sera ya uislam “ kutoa ni sera ya uislam na kutoa chochote ulichoruzukiwa kiwe kidogo au kikubwa” alisisitiza sheikh Simba.

Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni17321300, zilikusanywa, fedha taslimu zikiw a milioni 4881300 na milioni 12,404,000. Vifaa vya ujenzi vilivyotewa saruji mifuko 87, mchanga maroli 6, bati 6.

Nae mkuu wa wilaya ya Geita ndugu Philemoni shelutete, akitoa salam za wilaya katika harambee hiyo alisema anaunga mkono jitihada za waislam wa Geita na kuhaidi kuwasaidia kwa hali na mali kwani kuanza kwa shule hiyo kutaleta manufaa kwa waislam na wasiokuwa waislam, na hatimaye kutoa ahadi ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja.

Shule hiyo inayomilikiwa na Bakwata, wilaya ya Geita, ilianza ujenzi wake mwaka 2007katika eneo la Mwatulole, kijiji cha ihabuyaga kata ya kalangalala, mjini Geita.

Kukamilika kwa ujenzi wa Shule hiyo ya bweni inaweza kumaliza tatizo lililopo wilayani hapa la wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na kufaulu baadhi yao wanakosa nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari na wasichana wanaochaguliwa katika shule za sekondari kukosa sehemu za kulala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ndio, lazima tuige jinsi wayahudi walivyoweza kuvishinda vitisho vya hitler na wenginewo.

    ReplyDelete
  2. at last,point imewekwa,mana hatuishi kulalama weee
    ooo sijui wakristo wanapendelewa nk nk,tusomeni jamani tuelevuke na tuendelee,,sio kukalia kubebwa-bebwa
    tusomeshe watoto wa kike na kiume wa kiislam elimu bora

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...