Ankal pole na kazi za kuelimisha jamii. Tunaomba utuwekee katika glob yetu ya jamii ili maombi yetu yasikike kwa wahusika, maana tunajua haakosi kutupia jicho humu.

Sisi tulikuwa wanafunzi wa chuo cha elimu ya biashara CBE Dar es Salaam
tumemaliza mwaka 2006 wengine mwaka 2007 na tulifaulu katika masomo tuliochukuwa Ajabu mpaka leo huu mwaka wa nne hatujapata vyeti vyetu muda tuliosoma ni miaka mitatu ni ajabu muda wa kusubiri vyeti unazidi muda wa masomo na kila kukicha ni sababu tuu, mara printer hajapatikana, mara vinachapishwa nje ya nchi ili mradi siku zinakwenda ikiwa na ada tulishalipa tukamaliza tena kwa wakati.

Hii inatupa shida hata tunapoomba kazi wanakuwa na wasiwasi kama kweli tulisoma hapo maana tunatumia transcript ambazo wengine hawazikubali na hata iwapo unatakiwa upande cheo mwajiri anasema lete cheti chako kama huna unabaki palepale ulivoajiriwa na cheti cha awali.

Wadau wa enzi CBE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ningekuwa mimi ni Mamlaka ya uteuzi na utenguzi wa Wakuu wa Vyuo Vyote VIkuu vya Umma. NIMETENGUA UTEUZI WA WAKUU WA VYUO VYOTE [kuninge wanaitwa Makamu Mkuu wa Chuo] ningefuta uteuzi wao na ningechagua wengine kutoka Nje ya Taasisi hizo.

    ReplyDelete
  2. Anon wa kwanza, kwa sababu zipi?
    Poleni wadau wa CBE. No wote au kuna wengine wanapata? 'Chai' Haihitajiki hapo?

    ReplyDelete
  3. Ninakubaliana na mlalamikaji kuhusu uzembe wa CBE. Mimi nilikuja huku nje ya nchi kuendelea na masomo yangu lakini cha ajabu ni kwamba kila nikiomba matokeo yangu kutoka CBE ninapewa kila sababu ya kutopewa majibu hayo. Nilipokuja kuomba 'course description' ya masomo ili niweze kupata credit kwa baadhi ya masomo, CBE wakasema kwamba hawatoi information hiyo mpaka Chuo changu hapa kiombe rasmi. Chuo changu kilipotuma barua ya kuomba information hiyo, barua ilirudi kwani hakuna aliyejishughulisha na barua hiyo.
    Haya ni mambo ya ajabu sana kwani wenzetu wanshangaa sana inakuwaje ni vigumu kupata hata 'course description' ya masomo kutoka kwenye chuo kwani information hiyo huwa inapatikana hata kwenye syllabus au prospectus.
    Uzembe wa hali ya juu sana uko hapo CBE na ni aibu kubwa sana. Wengine tungependa kusaidia chuo chetu cha zamani lakini kwa mtindo huu ni bora nikatoe msaada wangu kwenye shule na vyuo vingine kwani nina uhakika kwamba hata mtu ukitoa msaada utaishia mifukoni mwa wachache wenye madaraka na uzembe.

    ReplyDelete
  4. Nilikuwa Dar Tech miaka ya tisini Mwishoni ambapo tulikuwa tunaenda kujirusha siku ya Ijumaa kwenye baa hapo CBE. Mambo yalikuwa Mswano hasa walipokuwa wakialika Bendi mbalimbali. Kwa burudani walijitahidi, lakini sikujua kuwa Kiutawala CBE kuna uzembe na uozo wa namna hiyo. Shame on them!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...