Waambaje kaka michuzi!
mimi ni mdau wako wa siku nyingi ila si mchangiaji sana.....mara nyingi mimi huwa nasoma na kuangalia post zako tu. Lakini kuna mambo machache yananikereketa kuhusu hawa TANESCO na mgao wao.
La kwanza ni kuhusu ratiba ya mgao wa umeme. Unajua walipotangaza kuhusu mgao wa umeme waliahidi kutoa ratiba ya mgao huo ambayo waliitoa kwenye vyombo vya habari hususan gazeti la Mwananchi ambayo niliiona mimi.
Sasa cha kushangaza ni kwamba hiyo ratiba haifuatwi na kama kuna ratiba mpya na ile ya zamani haitumiki mbona hawaitoi? La pili ni kwanini huu mgao uwe unatekelezwa wakati mwengine wowote isipokuwa usiku mkubwa?
Kule kwetu Mtoni maeneo ya sabasaba ratiba haitambuliki, siku nyingine umeme unawashwa kwa mda wa saa 1 na siku nyingine inakuwa kama disco light.... zima washa zima washa tena saa za usiku mkubwa na huo mchezo wa kuzima na kuwasha ni baada ya mda wanaotaka wao. Sasa swali langu ni hivi...sisi wananchi wa Mtoni hatuna umuhimu wa umeme japo kidogo?
Cha kusikitisha umeme huo huo umeleta kero ya maji, leo asubuhi maji yalikuwa hayapatikani na sababu. Maji tunayototumia ni kisima ambacho kina pump ya kusukumia maji na pump hiyo inatumia umeme. Jamani Jamani haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania?
Hivi serikali hii hadi lini itaendelea kuwatesa wananchi wake? Sisi tuliowaweka nyinyi madarakani kwa kura yetu ndio mnatufanyia hivi? Jamani mtufikirie nchi za wenzetu wanasonga mbele kwanini sisi watanzania tunarudishana nyuma. ILI MAENDELEO YAJE INABIDI UMEME UPATIKANE!
La tatu....Kwanini hili tatizo la uhaba wa maji unaopelekea upungufu wa uzalishaji umeme halitafutiwi ufumbuzi na suluhisho la kudumu? Hivi kuna siku hii nchi itondokana na mgao wa umeme?
Mnaimaliza hii nchi!
Wako mdau Mama K wa mtoni.

Inasikitisha kuona wananchi wanateseka kiasi hiki,halafu utasikia viongozi wa serikali wanasema uchumi wa nchi unakuwa.Hakuna dunia ya nchi ambayo inamaendeleo bila ya kuwa na umeme wauhakika.Nimekaa nje ya nchi kwa muda wa miaka kumi bila sijawahi kukatikiwa na umeme au maji hata siku moja.Sasa leo hapa Tanzania kama serikali inashindwa kuwapa wananchi mahitaji muhimu kama Maji na Umeme na kila mtu kutumia generator hakuna haja yakuwa na tanesco.
ReplyDeletesisi nchi hii tumesha kufa na kupelekwa motoni,tukifa kweli Muumba atatusamehe kwani adhabu tutakuwa tumesha ipata...maisha gani haya! ahh!
ReplyDeleteYani nyie mmesahau kwamba Tanesco ni shirika la umma wanfanya kazi kwa manufaa yao na siyo kwa manufaa ya Mtanzania. Tutakaa gizani mpaka siku tutakayotambuwa haki zetu na kuzifuatailia. Michuzi usibani hii kwani hata wewe unaishi gizani pia. Hakuna anestahili kuwa na nyaya nyumbani kwake kama urembo. Next time mwananchi msilalamike huku kwenye mitandao, kinachohitaji ni kijuuliza tuwasaidie namna gani hawa Tanesco waliopotea, kwani wao wameshakula pesa wameshiba, sisi walalhoi ndiyo tunaoteseka. Kama unataka kupata umeme kwa uhakika nenda kaishi karibu na kiongozi wa nchi kwani kwenye line zao umeme huwa haukatiki, au nenda kaishi karibu na kituo cha jeshi line zao hazikatiki. Usilalamike leteni njia mpya ya kujisaidia sisi wenyewe. Tanesco wameshakuwa mafisadi tu.
ReplyDelete