MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMED GHARIB BILALI AKIKUTANA NA UJUMBE WA WAWEKEZAJI KUTOKA KAMPUNI YA SICHUAN HONGDA AMBAO NDIO WALIOSHINDA ZABUNI YA KUENDELEZA MIRADI YA MAKAA YA MAWE YA MCHUCHUMA PAMOJA NA CHUMA KULE LIGANGA.
MAKAMU WA RAIS AMEWATAKA WAWEKEZAJI HAO KUHAKIKISHA KUWA MIRADI HIYO INALETA TIJA KWA TAIFA LA TANZANIA. AIDHA DR BILAL AMESIFU JITIHADA ZINAZOFANYWA NA SHIRIKA LA TAIFA LA MAENDELEO-NDC KATIKA KUENDELEZA MIRADI MBALIMBALI KWAAJILI YA UCHUMI WA NCHI NA KUWATAKA WAWEKEZAJI HAO KUTUMIA FURSA HIYO KUTEKELEZA KWA UFANISI MIRADI HIYO
KWA UPANDE WAKE MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA TAIFA LA MAENDELEO DR CHRISANT MZINDAKAYA AMEMWELEZA MAKAMU WA RAIS KUWA KWA SASA MAJADILIANO YANAENDELEA KWAAJILI YA KUANZA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI HIYO NA PINDI ITAKAPOKAMILIKA UTEKELEZAJI UTAANZA MARA MOJA
KAMPUNI YA SICHUAN HONGDA NI MIONGONI MWA MAKAMPUNI YALIYOOMBA ZABUNI YA UETEKELEZAJI WA MIRADI HIYO KATI YA MAKAMPUNI 42 NA KUFANIKIWA KUSINDA ZABUNI HIYO.
NA NEEMA MBUJA
AFISA UHUSIANO MWANDAMIZI-NDC
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...