Wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania jijini New York, Marekani, wikiendi hii wamemuaga mwenzao Ndugu Omary Mjenga, ambaye ameteuliwa kuwa Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Miradi na Huduma- UNOPS, FreeTown, Sierra Leone.Kaimu Balozi Ndugu Justin Seruhere akimkabidhi Ndugu Mjenga na mkewe Asha zawadi iliyoandaliwa na wafanyakazi wenziwe.

Ndugu Mjenga, mkewe Asha na binti yao Kelly wakikata keki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi, Mjengwa? Nadhani Mjenga, kalamu huteleza!

    ReplyDelete
  2. Kila la kheri Ndugu Omary. Peperusha bendera.
    Swali, Mbona UNOP hawana cheo cha Mwakilishi Mkazi,(Resident Representative), huko Sierra Leone? Hii imekosewa ama ni cheo kipya kinaundwa?

    ReplyDelete
  3. Naam Hongera Mjenga. UN panueni wigo kwa Watanzania wenye uwezo na ujzi wapate nafasi hizi na sio tu kutoa kwa ukaribu fulani na Dr. Migiro.

    ReplyDelete
  4. Anon hapo juu 10:10:00 PM, acha majungu! Msherehekee Mjenga bila dukuduku. Nawe omba kazi upimwe kwa uwezo wako na sio ukaribu na mtu yeyote. Mbona una mpiga kijembe mtanzania mwenzako?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...