MV Magogoni likila mzigo upande wa Magogoni. Geti lake moja limepata mushkeri na huenda lisianze kazi mapemba asubuhi kesho hadi baada ya matengenezo
MV Kigamboni likiwa mzigoni. Kesho asubuhi ndilo linategemewa kuwa mkombozi wa wana Kigamboni. Pembeni yake ni MV Alina ambayo nayo huokoa jahazi mambo yakienda mrama

Habari zimeingia sasa hivi toka feri jijini Dar zinasema kwamba geti moja la pantoni ya MV Magogoni limekatika ikiwa njiani kutoka Kigamboni kuelekea Magogoni na kizaazaa cha aina yake kimeripotiwa baada ya abiria kuvamia maboya ya kuzuia kuzama ili kujinusuru. Bahati nzuri pantoni ilifika salama ng'ambo ya mjini na abiria kushuka salama bin salimini.

Hata hivyo wachunguzi wa mambo wameiambia Globu ya Jamii kwa sms kwamba ni MV Kigamboni pekee itakayoanza kazi kesho asubuhi na kutabiri foleni ya kufa mtu pamoja na kuchelewa wadau makazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wabongo bwana!

    Yaani nayo mara hii tayari wameshaanza KUICHAKACHUA!

    Khaah!

    ReplyDelete
  2. Daraja lazima itengenezwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...