Waziri wa Miundombinu, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mthamni Mwandamizi wa Wilaya ya Kinondoni, Einhard Chidaga, wakati alipokuwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Ubungo Maziwa, inayotokea Kigogo, wakati wa ziara hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, wakati huo huo Waziri huyo ametoa siku tano kwa Meneja wa Mkoa kubomoa ofisi yake iliyopo Ubungo, ili iwe mfano kwa raia wengine wanaotakiwa kupitiwa na zoezi hilo la ubomoaji ili kupisha upanuzi wa Barabara na mradi wa Magari yaendayo kasi. Picha na mdau Muhidin Sufian.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi magari yaendayo kasi ni nini???au ni nchi gani duniani inayatumia??

    ReplyDelete
  2. TO BE HONESTY MIMI SIIPENDI CCM, ILA KAMA ITAMSIMAMISHA MAGUFULI KUGOMBEA URAIS 2015 KURA YANGU AMEIPATA BILA KIPINGAMIZI.

    ReplyDelete
  3. nadhani ni mabasi yaendayo kasi BRT( BUS RAPID TRANSIT) mabasi ya DAR yatajulikanan kama DART, ( DAR ES SA LAAM RAPID TRANSIT) yanaitwa mabasi yaendayo kasi sio kwa sabbau ya mwendo wake wa kasi au HIGH SPEED, ni kwa sababu yanakua na barabara yake BRT LANE , Ambayo magari mengine hayataruhusiwa kupita katika lane hiyo, hivyo kuyafanya mabasi hayo kutokua na folenina kuwa ya haraka.
    kwa kujifunza zaidi tembelea hapa
    http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=1191319
    http://www.chinapage.com/transportation/brt/bjbrt.html
    http://thecityfix.com/wp-content/uploads/2008/05/lagos4.jpg
    na hapa pia http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=430948&page=41

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...