Ngosha alijiunga na DDC Mlimani Park miaka ya mwanzoni ya 90, akiwa anajulikana kama Charles John Ngosha ila baadae alibadili dini na Kuwa muislam na kupewa jina la Mustafa. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana,Ilala jijini Dar.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Tandale kwa Popobawa jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa mmoja wa wanakamati ya mazishi na mwanamuziki mkongwe Hassan Rehani Bitchuka, mazishi yatafanyika leo saa saba mchana. Ngosha, aliyezaliwa mwaka 1965, ameacha mke na watoto 10
M.Ngosha (RIP)Sikinde imepoteza msanii mkubwa...
ReplyDelete/Mdau Vumbi Dekula Sweden
Kalale pahali pema peponi Ngosha,
ReplyDeletewewe ndiye uliyekuwa"Ngouma Lokito"
wetu tanzania,utakumbukwa na kuheshimiwa daima kwa upigaji wako mahiri wa bass.Pia shukrani zangu kwa wanamuziki wenzetu wote mlioko nyumbani Tanzania kwa kuwa na moyo wa upendo hasa wakati wa misiba ya wanamuziki wenzetu sisi tulioko nje
ya nchi hufarijika sana tunapowaona mkishiriki ktk.misiba hasa kupitia mitandao mbali mbali,Nawapa pia pole kaka zangu wa Sikinde."Respect"
Abbu Omar,Prof.Jnr(mwanamuziki)Tokyo,Japan.