Mkuuwa wilaya ya Geita Mh. Philemoni Shelutete, (kati) akimpokea Sheikh mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Bin Shabani Simba, (shoto) katika ikulu ndogo ya Geita. Kulia ni Sheikh mkuu wa wilaya ya Geita Sheikh Haadi Kabaju. Mufti Simba, anatarajiwa kuongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenziwa shule ya kiislamu wilayani humo leo.
Umati mkubwa wa waumini wa Dini ya kiislam, wa geita, wakishiriki maandamano maalum yalioandaliwa kwaajili ya kumpokea Sheikh mkuu wa Tanzania, Sheikh issa Bin Shabani Simba, aliyewasili jana mjini hapa, Sheikh Simba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kiislam ya Geita, harambee hiyo itafanyika leo hapa Geita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nimefarijika sana kusikia kuwa Sheikh Simba ataongoza harambee ya kuchangisha fedha za kujenga shule. Ndiyo, tunahitaji shule zaidi.

    ReplyDelete
  2. Shukrani kwa waislam wa Geita na Mufti mkuu kwa kulion hili. Waislam wanachotakiwa ili kuboresha maisha yao na watoto wao ni kuzingatia elimu bila hata kuadhiri imani yao. Mimi kama mkristo ambaye liberal ambaye nimekuwa na kusoma na waislamu ambao wengi wamekuwa rafiki zangu wa hali na mali, adui wa uislam sio ukristo bali hali iliyokuwepo ya kutozingatia elimu ya shuleni.

    Napata faraja kwamba sasa wameanza kiliona hili, na nimatumaini yangu waislam wote nchi watafuata mfani huo wa ndugu zetu wa Geita, ili kwamba nchii hii iendelee bila ya kuacha jamii fulani nyuma.

    Hongereni Waislam wana Geita

    ReplyDelete
  3. Wewe pumbavu uliyesema waislamu hawazingatii elimu ya shuleni, nakuuliza umesoma shule gani na miaka gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...