Sisi watoto wa marehemu Brigedia Jenerali (Mstaafu) William Stephen Kotta, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ndugu, marafiki, majirani na jamaa wote walioshiriki katika msiba na mazishi ya mpendwa baba yetu William Stephen Kotta aliyefariki dunia tarehe 6 Desemba 2010 na kuzikwa tarehe 10 Desemba 2010.
Shukrani zetu za dhati na za kipekee ziwaendee;
-Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ) Jenerali Davis Mwamunyange
-Viongozi, wafanyakazi , makamanda na wapiganaji wa JWTZ
-Canon Soseleje na waumini wote wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Martin, Kawe
-Uongozi wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano, Upanga
-Mkuu wa Makampuni ya IPP, Bw. Reginald Mengi
-Uongozi wote na wafanyakazi wa Radix Gear Ltd.
Si rahisi kwetu kumshukuru kila mmoja au kikundi lakini tunawasihi tangazo hili litosheleze na kuwa shukrani zisizo pungufu kwa wale wote ambao hawakutajwa.
Arobaini ya marehemu itahitimishwa kwa ibada(Misa) itakayosomwa Jumamosi tarehe 15 Januari 2011 saa 4.00 Asubuhi, nyumbani kwa marehemu Kunduchi, Kilongawima.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Ndugu zangu poleni sana kwa msiba huu, Bwana ndiye mpangaji wa kila kitu na tunaamini kazi yake haina makosa, Sikuweza kuhudhuria niko mbali ila tuko pamoja sana katika maombi.
ReplyDeleteJames Sekwao