Familia ya Marehemu Mwalimu Julius Banzi wa Kiwanja cha Ndege-Tangi Bovu Morogoro, inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kumuuguza na hatimaye katika kuifariji familia wakati wa msiba wa mpendwa wao Mwalimu Innocentia Banzi, aliyefariki tarehe 12.01.2011 na kuzikwa tarehe 15.01.2011 katika makaburi ya Kola-Morogoro.
Kwa kuwa si rahisi kuwataja wote, familia inapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani kwa Madaktari na wauguzi wote wa hospitali za Mkoa Morogoro; Ocean Road; na TMJ-Mikocheni: Pia tunaishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi; Wakuu wote wa shule za sekondari Tanzania; Vyama vya Msalaba Mwekundu na Skauti-Tanzania; Jumuiya za Watanzania Finland na Uingereza; na Mabloger wote waliotusaidia kupasha habari za msiba huu.
Shukrani za pekee pia ziuendee uongozi wa katoliki parokia ya Roho Mtakatifu-Kiwanja cha Ndege, Morogoro; Mtakatifu Petro Oysterbay: na Mtakatifu Theresia Mbezi Luis, kwa msaada wa kiroho.
Tunaomba wote mzipokee shukrani zetu hizi za dhati na kwamba Bwana awabariki kwa moyo mliounyesha kwa familia.
Mkesha wa msalaba utakuwa tarehe 28.01.2011 kuamkia tarehe 29.01.2011 (Jumamosi) ambayo itakuwa ni siku ya msalaba wenyewe.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
[Ayub. 1:21]

Samahani, kwa anaye fahamu - kuna wakina Banzi walioishi kule UDSM wanaweza kuwa na undugu? Kuna mmoja (Clemence), tulisoma naye pale UDSM, na kaka yake alikuwa akifanya kazi maktaba ya UDSM kipindi hicho hicho. Mungu awatie nguvu na kuwafariji wafiwa.
ReplyDeletepoleni sana wafiwa. kuna dada nlisoma nae chuo cha ualimu 2001-2 anaitwa Esther Banzi na alikuwa anaishi morogoro, nahisi kama ana undugu na huyu marehemu kwani wanafanana sana. poleni sana wafiwa wote Mungu awatie nguvu.
ReplyDeleteMpendwa uliyeuliza kuhusu Esther..huyo Esther ndo yeye na huyo ni Mama yetu tena Mzazi sio ndugu wa kawaida tu ni mzazi wetu. Asante tulimpenda sana Mama yetu lakini Mungu kampenda zaidi yetu.Jina la bwana libarikiwe.
ReplyDeletePoleni sana watoto na ndugu wote wa mama Banzi, Mwalimu wangu huyu alinifundisha Morogoro Sekondari (Moroseco). Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi ameni.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa. Mwenyezi Mungu awepe nguvu katika kipindi hiki kigumu. Namkumbuka sana mwl Banzi, alikuwa mwalimu wangu wa michezo morosec. R.I.P MWL BANZI
ReplyDelete