Napenda, kwa kupitia blogi yako niwashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zangu kokote duniani katika wiki hii ya kukumbuka miaka 5 ya ndoa yetu. Ilikuwa ni miaka mitano iliyopita, jijini Dar Es Salaam, tuliporasimisha mahusiano yetu, ambayo yalidumu kwa miaka zaidi ya 5 kabla ya ndoa.

Tunamshukuru MUNGU kwa yote aliyotujaalia, kwa baraka zake, tumekuwa na kutambua na kuthamini sana maisha ya "wawili': (samelife): ndoa ni baraka, kwa sala na maisha ya mfano, mwenyezi Mungu humjaalia na kumpa mke/mme mwema. Pia kwa namna ya kipekee tunamshukuru MUNGU kwa baraka za kupata watoto: ndoa yetu imejaaliwa watoto wawili: Vania-Liv (3.7 ysr) na Gaven (13m). Wote wana afya njema, na wanawasalimia ndugu na jamaa yote kokote duniani:

Kuanzia Kobe hadi Hawaii, Siberia mpaka Cape Town, Santiago mpaka Vladivostok pia kutoka Wellington mpaka Juneau tunasema asanteni sana. Orodha ya ndugu waliofanikisha harusi mnamo January 2006 na pia ndugu walioishi nasi, kutupa sapoti mbalimbali ni ndefu, tunaomba kwa wale wataopata nafasi ya kusoma hapa kwa Blogi ya Jamii wapokee asante yetu na watufikishie kwa wengine wote: Asanteni Sana.

Edmund Matotay na Josephine Duway



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hongereni sana wapendwa. Mungu na ailinde ndoa na familia yenu ( Shetani aiangalie kwa mbali tu). Nice pics. Cute family. Mary,The Hague

    ReplyDelete
  2. Hhiyaee kungaa mungu nu tsuqi.Aning aga loawa qwalaa kunga nuwa barakawaa ar, aning loarbaradori an kungawa firiim nu slaaririi doog.
    MICHUZI HUYU NI NDUGU YANGU NAOMBA USIWEKE KAPUNI HII COMMENT YAANI HUYU JAMAA YANGU AKISOMA HII ATAFURAHI SANA.

    ReplyDelete
  3. Hongereni sana Edmund na Josephine, Mungu awaongezee baraka na kuilinda ndoa na familia yenu. Mdau Frogner, Norway

    ReplyDelete
  4. Hongereni sana Fina na Eddy. Endeleeni kumtanguliza Mungu kwa kila Jambo. Vi Glatulerer.

    ReplyDelete
  5. Hongereni sana ila mi nina angalizo... hapa mmetueleza kuwa Mungu kawajalia watoto, sasa mbona mmejiweka wenyewe tu? angalau mngeweka picha ya pamoja na hao watoto basi..

    ReplyDelete
  6. (Kuanzia Kobe hadi Hawaii, Siberia mpaka Cape Town, Santiago mpaka Vladivostok pia kutoka Wellington mpaka Juneau tunasema asanteni) sana.Hao ndugu zako hakuna wanaopatikana Tanzania????

    ReplyDelete
  7. Hongereni sana the Matotay's....It's unbelievable kwamba miaka mitano tayari....Mungu awazidishie maisha mema na yenye furaha,...na marefu pia....usisahau kula "Melange med brød og hønning"!...det var din favoritt i gamle dager!!!

    ReplyDelete
  8. hapa ni miaka kumi ya ndoa sio mitano. Unless hatujui maana ya ndoa maana wenyewe wameshasema walikuwa pamoja kabla ya hapo na walirasimisha tu mwaka huo!

    Kweli ndoa ni ngumu, miaka mitano yote hiyo? but mna bahati, ni wangapi wanaishia kuwa vidumu? nashari wadada wenzangu kuwa macho sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...