kwanza habari ya mwaka mpya kaka na wadau hapo bongo,
wadau hapa kuna swali la utata kuhusu mwafrica au mtu mwaeusi kwa ujumla,
hivi ni kweli hatujapewa kipaji chochote na mwenyezi mungu zaidi ya kucheza ngoma na kuimba???

mkasa mwenyewe ni huu,ukiangalia dunia nzima kuanzia mzungu,mchina,muhindi na mtu yeyote yule ametuacha mbali waafrica kwanini???

je tukimaliza ubishi wa kubadilisha nchi wajerumani wachukue Tanzania,watanzania wachukue Ujerumani na kila kilchopo ujerumani,swali baada ya miaka mitano nani atukuwa juu kimaendeleo????

ni wajerumani waliochua tanzania au watanzania waliochukua ujerumani????
jibu,wajerumani waliochukua tanzania ikiwa masikini watakuwa na maendeleo,utaona metro,trams,trein za umeme tanzania nzima,haya tuangalie watanzania waliopo ujerumani,kwanza Raisi keshauza luftansa,na utashaangaa mgogo.

anafunga ngombe gorofani humburg,utaona mzalamo anatwanga mpunga golofa ya saba nane usiku,matrein yote yamekufa; mlugulu analima mchicha kwenye underground za metro,ni hivyo hiyo na wakenya wakipewa uingereza baada ya miaka mitano; kila kitu kimekufa,na utaona waingereza wanaendela kenya,mwisho tunaanza kurudi africa kuomba kazi.

Je kweli mtu mweusi zoba?????
mdau ulaya....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Yes, wewe ni zoba b'se u wish u were mwingereza au mjerumani.We don't live in hypothetical world....

    the question is: what is your contribution? kulalamika haukotoshi..

    ReplyDelete
  2. mmh mdau wa kwanza acha uzushi lakini mdau wa ulaya si amesema kweli? kwani air tanzania iko wapi? angekuwa meneja ni mzungu ndege zetu zingeruka hadi new york city leo haziendi hata hapo zanzibara ukweli unachonyota eehh, na mbona daraja la hapo kigamboni danadana tuuuuuuu angekuwa ni mzungu jeee tunazaliwa tungekuta daraja lipo, achana na ngozi nyeupe thinking capacity yao iko juuu sana full maendeleo ufisadi 0%, kubali kataa ukweli ndo huo na habari ndi hii

    ReplyDelete
  3. Ututake ladhi fara wewe!........Maendeleo yote unayoyaona huko Europe yametokana na UHARAMIA wa kuiba rasilimali za Africa na nguvu kazi yake...................stop that pleas

    ReplyDelete
  4. Fikra kama hizi ndiyo madhara yatokanayo na ukiristo. Yesu mwana wa mungu mweupe (hivyo baba yake mzazi pia atakuwa mweupe); malaika wa mungu weupe, lakini shetani (aliyelaaniwa na mungu) mweusi.

    Sasa kwanini watu weusi wasijichukie.

    ReplyDelete
  5. Hili swali linagusa mambo mengi sana ya kibaiologia, kisaikologia, kiuchumi, n.k. na sidhani jibu lake ni rahisi tu kama mtoa mada anavyooelezea. Kwanza ngoja nikanushe baadhi ya mada ulizojadili. Si kweli kwamba wajerumani wakija Tanzania miaka mitano tu watajenga maghorofa, treni za umeme, n.k. nchi nzima. Huu si ukweli. Kama ni kweli basi Afrika Kusini ambako wazungu walitawala kila njia za uzalishaji mali kungekuwa sawa na Ujerumani. Pia kumbuka kwamba kuna nchi kibao zenye wazungu ambao hadhi zao ni za chini kuliko nchi kadhaa za kiafrika. Kwa mfano, Botswana, Gabon, na Namibia zimeendelea zaidi ya nchi nyingi tu za Ulaya Mashariki (Albania, n.k.) na Asia. Hivyo hoja yako ya uafrika haiwezi kukubalika moja kwa moja. Pia ziko nchi kibao zenye watu wenye asili ya kiafrika ambazo zimeendelea sana tu. Fikiria hili: Ukichukua wamarekani weusi au weupe wa Albania uwabadilishe na watanzania, ni kundi gani litaleta maendeleo haraka?
    Kwa maoni yangu, jibu la swali lako linagetemea mambo makuu matatu:
    (i) Ubaguzi wa rangi: Mataifa mengi ya Asia na Amerika ya Kusini yameendelea kwa sababu ya fedha za uwekezaji kutoka mataifa yaliyoendelea. Nchi zilizoendelea haziwekezi katika nchi za kiafrika kama walivyofanya kwa mataifa ya Asia (ii) Ukoloni: Watu wengi hawaelewi jinsi ukoloni ulivyosababisha vita vya ndani kwa ndani katika mataifa mengi ya Afrika. Ukoloni ulileta mfumo tofauti wa kijamii na kiuchumi ambao jamii nyingi za kiafrika zilikuwa hazijajiandaa kuingiza kwenye mifumo yao. Vita na migogoro imechangia kurudisha nyuma maendeleo na pia kuwafukuza wawekezaji ambao wangesaidia kuinua chumi za nchi nyingi (iii) Utamaduni: Utamaduni wa jamii zetu ni wa kijamii na kusaidiana na sio wa kibinafsi kama wenzetu. Bahati mbaya misaada ya kijamii mara nyingi inadumaza ubunifu na kuongea uzembe. Hili limetokea kwa sababu bara letu limekuwa likijitosheleza kwa chakula kwa karne nyingi kabla wavamizi hawajaingia. Hivyo hatukuwa na sababu ya kujenga dhamira ya maendeleo ya kibinafsi ambayo mara nyingi ndio chocheo la maendeleo ya jamii kwa ujumla.

    Senti zangu mbili.

    ReplyDelete
  6. Ha mbona una mawazo finyu. Kwani kila kitu kinachofanywa na wazungu kinaendelea? Mbona kuna mengi tu yamewashinda. South Africa huko kuna wazungu wanaishi kama Tandika. Romania wanaomba waje Bongo kuishi. Kufanikiwa au kutofanikiwa ni bahati ya mtu, unaweza ukafanya kazi kwa bidii lakini ukala hasara, ukakosa wateja. Kuna jimbo huko USA sawa na Tanzania kwa umasikini.

    ReplyDelete
  7. Binadamu wote tuna akili sawa. Tatizo ni mtazamo wa maisha (attitude) na historia. Tumekwishajijengea "attitude" ya kutofikiri kuhusu kesho na kesho kutwa na pia kujifikiria binafsi kuliko kufikiria maslahi ya jamii zetu. Tutakapobadili "attitude" hiyo, ndipo maendeleo ya mtu mweusi yataanza.

    ReplyDelete
  8. Hii ni kweli kabisa,na hata walichoacha wajerumani tunamalizia kwa kuiba na kujigawia tu,we are greeedy,angalia majibu kwenye you tubePastor DR James David Manning ,ndio yale yaleee,jamaa kauliza swali wengine mnataka kumchapa makofi humu,nyumba wanaokaa ma RC,mawazili,barabara dar,bandari vitu muhimu vyote waliacha wazungu,sisi tumejenga nini?hadi leo umeme tu umetushinda??

    ReplyDelete
  9. Mi sidhani kama mdau ulikuwa ana maana ya kuuliza swali cha muhimu alikuwa anajaribu kuelezea kwanini hatuendelei???Hivi misaada mingapi imefika Tanzania?achana na wakenya,at least wao wanaendelea japo ubaguzi wao wa kikabila mmh...,kinachoboa bongo ni k1 tu ubinafsi umezidi,watu hawafanyi kitu kwa faida ya jamii inayomzunguka na mbongo ana uwezo wa kufkiria finyu sijui tuseme?kingine dah tungejua jamani haya mambo ya mafisadi zamani ingekuwa afadhali sasa may b,nashindwa kuelewa kwanini wanasiasa ni pekee wa kibongo ndio wanaolipwa ngawira nyingi kiasi ukitaka kuwa tajiri lazima uwe mwanasiasa kwanza?itafikia wakati kila mtu mwanasiasa,angalia sekta kama za michezo wenzetu hata huko zinalipa,ila bongo uhasibu tuuuu na uanasiasa sasa nchi nani ataiendeleza?walimu wabovu huko ngazi za chini,mtu amefeli ndio anaenda ualimu na hiyo inachangia coz mshahara mdogo nani ataenda fanya hiyo kazi?madaktari hovyoo yani wamechooka hivi lini watakuwa creative na tiba zao?maengineer ndio vile tena mpk kujuana kazi ndio wapata,hivi lini itakuwa watu wanafanya kazi kwa kujua ukiharibu wenzio wanaisubiria?nani atabadilisha mwelekeo kama si wewe unayesoma hivi sasa?badilika kwanza wewe then watafuata tu watu,cha kwanza tuondoe mfumo mbovu wa kisiasa,serikali isiwe ndio kila kitu at least yale mashangingi wasipewe basi ili wakigombea wasitoe sana rushwa tupate viongozi makini wataokuwa wanaweka maslahi ya nchi mbele,aah hata sijui niandike mangapi yataweza kueleweka maana ni mengi na inauma ukifikiria maana we have a very looooooooooooong way to GO!

    ReplyDelete
  10. Anon 12.05 acha uongo wa kitoto,unasema kuna jimbo USA maskini km TZ,ok litaje hilo jimbo kwa jina na unatumia vigezo gani kusema Hilo jimbo nimaskini km TZ?do some research my poor friend,angalia per capital income of that state and then compare with that of TZ go on to see how much the min pay rate and compare to that of TZ then proceed to compare social developments-utilities,medical,infrastrucure,schools etc. Acha kudanganya watu bwana mdogo

    ReplyDelete
  11. SWALI LA KIZUSHI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...