Kwanza nikupe pongezi sana kwa kuendelea kutuhabarisha kuhusu matukio mengi yanayotokea huko nyumbani na duniani kwa jumla. Mimi binafsi ni mmoja wa watu ambao hatukosi kusoma globu yako kila siku.

Kwa muda mrefu niliona mjadala wa nini maana ya neno libeneke ambapo watu kadhaa walijitokeza kuchangia. Kutokana na shughuli nyingi sikuweza kuchangia mapema zaidi ya leo.

Napenda wasomaji wako waelewe kuwa libeneke zaidi ya kuwa mtindo wa muziki wa dansi uliokuwa unatumiwa na Bendi ya Muziki wa dansi ya iliyokuwa inaitwa KILOMBERO JAZZ BAND na baadaye kubadilisha jina na kuitwa BUTIAMA JAZZ BAND, asili yake hasa ni moja ya ngoma za kabila la Wandamba waishio wilayani Kilombero, Mkoa wa Morogoro. Nyimbo zao nyingi kama Monike na zinginezo nyingi ziliimbwa kwa lugha hiyo.

Kwa leo sina mengi zaidi.
Nakutakia kazi njema.
Mdau Geneva

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwa kuongezea ningeomba wadau mumuone mzee Alphonse Makello,mwanamuziki mkongwe kwa sasa kama sikosei yupo Shikamoo Jazz,Yeye ndiye aliyekuwa mpiga Solo na kiongozi wa Kilombero Jazz na baadae Butiama Jazz,yupo Dar na anapatikana maeneo ya Buguruni.
    mdau Japan.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...