Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akiongea na ujumbe wa wawekezaji wa mradi wa uzalishaji umeme wa Liganga na Mchuchuma kutoka China wakati wa hafla ya chakula iliyoandaliwa na makampuni ya China leo kwa lengo la kuwekeza katika uzalishaji wa umeme ambapo amesema kuwa serikali imeshawapa maelezo ya kutosha yatakayowawezesha kuja nchini kuwekeza kwa wakati.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu akiongea na ujumbe wa wawekezaji wa mradi wa uzalishaji umeme wa Liganga na Mchuchuma kutoka China utakaojengwa kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na makampuni ya China leo jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...