TBF imeteua wachezaji na makocha wa timu ya Taifa kwa wanaume na wanawake. Makocha ni Evarist Mapunda na Tibeth Matiku kwa wanaume na Leornad Kwale akisaidiwa na Pasco Nkuba, Meneja wa Timu atakuwa ni Meja Specioza Budodi.

Pia TBF imeombwa kupeleka Kigali waamuzi wawili wa Kimataifa wenye beji za FIBA kutoka Tanzania watakaoshirikiana na wengine kuchezesha mashindano hayo, Kamisheni ya Waamuzi ya TBF itatangaza majina hayo baadae, Kamisheni ya Tiba ya TBF nayo itatoa daktari atakayemabatana na timu.

Timu ya Taifa inajiandaa na mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (kanda ya Tano ya FIBA Africa) yatakayo fanyika nchini Rwanda - Kigali tarehe 7/2/2011 - 12/2/2011, kwa sasa timu inafanya mazoezi katika uwanja wa ndani wa Taifa kuanzia saa kumi kamili Jioni kila siku za wiki.

Ni muda mrefu timu zet za Taifa za Kikapu hazijashiriki mashindano makubwa ya kimataifa yanayoshirikisha timu za taifa, na mwishoni mwa mwaka jana tulipata nafasi ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Comoro kwa ajili kujiaandaa na michuana hii.

Washindi wa juu wawili wa mashindano haya ya kanda ya 5 watapata nafasi ya kushiriki mashindano ya ya kuwania ubingwa wa mataifa ya Africa baadae mwaka huu. Hivyo Mashindano haya ni muhimu sana kwetu kushiriki.

TBF bado ipo katika mchakato wa kutafuta wadhamini kwa ajili ya kuwezesha safari hiyo ambayo gharama zake kwa ujumla ini shs. milioni 40 kwa timu zote mbili kugharamia usafiri kwenda na kurudi, malazi, chakula, ada za ushiriki na matumizi mengineyo.

Tunaomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, makapuni,Taasisi na mashirika mbalimbali kusaidia timu hii ili iweze kushiriki ipasavyo katika Michuano hiyo mikubwa katika kanda ya tano.

Ahsanteni

Phares Magesa

Makamu wa Rais (TBF)

---------------------------------

NATIONAL TEAMS 2011

(A) TANZANITE MEN TEAM:

POINT GUARDS:

1. Gerald Baru-Oilers 2 .Mohamed Yusuph-savio 3. Andrew Ikungura-Pazi 4. Sudi Abdurazak-Vijana(Uganda)

SHOOTING GUARDS:

5.Francis Mlewa-JKT 6.Mussa Chacha-Savio 7.Adamu Jegame -JKT 8.Robert Edward-Soweto king (Arusha)

SMALL FOWARDS:

9.Mohamed Ally –Vijana 10.Alpha Kisusi-Vijana 11.Denis Chibula-Pazi 12.Chelu Simion-Heats(Mwanza)

FOWARDS:

13.George Tarimo-Savio 14.Dogo Nyambura-ABC 15.Lusajo Samwel-Oilers 16.Jije Makani-Savio

CENTERS:

17.Gilbert Batungi-ABC 18.Mwalimu Kheri-Vijana 19.Mohamedi Makani-Changombe boyz 20.Juma Kisoky-ABC
RESERVE: 1.Benedictor Mwangara-Chui

TANZANITE WOMEN TEAM

POINT GUARDS:

1. Lucy Agustino-Jeshi Stars 2.Evodia kazinja –JKT Stars 3.Tukusubira David –Vijana Queens SHOOTING GUARDS: 4.Niphael Kessy-Jeshi Stars 5.Faraja Malaki-Jeshi Stars 6.Zakhia Kondo-Don Bosco

SMALL FOWARDS:

7.Jabu Shabani-Jeshi Stars 8.Doritha Mbunda-JKT Stars 9.Elizabeth Masenyi-JKT Stars 10.Sekela Dominic- JKT Stars

POST PLAYER:

11.Revina Julius-JKT Stars 12.Jackline Shemeza-Jeshi Stars
13. Annomisiata Anthony – Jeshi Stars
14. Nelly Anyengisye – JKT Stars
15. Nyilabu Maximillian – JKT Stars





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mbona Hasheem Thabeet hayupo kwenye team jamani? AU sio raia wa Tanzania?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...