Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb) akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman. Mihimili hii ya Dola ilikutana jana kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Spika Makinda akiwa safarini kwenda kisiwa cha Isle of Man kuhudhuria mkutano wa maspika wa mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola na Jaji Mkuu akielekea Zanzibar kuhudhuri maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Spika Makinda akimsikiliza kwa makini Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Mhe.Dkt. Cyril Chami (Mb) walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jana. Dkt. Chami alikuwa akitokea nchini India alikokuwa amefanya ziara ya kikazi.
Picha na Prosper Minja - Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...