Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu - Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi akiongea na waandishi wa habari na baadhi ya maafisa wa Tume ya Kuratibu na Kudhibiti Dawa za Kulevya Nchini pindi alipotembelea tume hiyo leo jijini Dar es salaam. Waziri Lukuvi amesema kuwa tume hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya kuthibiti uingiaji wa biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na udhaifu wa sheria iliyopo ya kupambana na kuthibiti dawa za kulevya ambapo amesema kuwa serikali itaunda timu itakayotoa mapendekezo kuhusu uimarishaji wa sera, muundo na urekebishaji wa sheria ya kudhibiti dawa za kulevya ya mwaka 1995 ili kutoa uwezo kwa Tume hiyo kuwashughulikia mara moja watakaojihusisha na biashara hiyo.
Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Christopher J. Shekiondo akitoa Taarifa ya utendaji kazi wa Tume ya Kuratibu na kudhibiti Dawa za kulevya kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu -Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi (kushoto) leo jijini Dare salaam ambapo ametoa wito kwa wananchi kuwafichua wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Baadhi ya wanahabari na maofisa wa Tume ya Kuratibu na Kudhibiti Dawa za kulevya wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu -Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi leo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. hivi haiwezekani kuwa kwa jinsi tunavyopiga vita madawa ya kulevya ndo biaashara yake inashamiri.
    mimi nafikiri kunahaja ya kuifanya halali tuone hayo mabilion watayatoa wapi.

    Mbona pombe,sigara na uzinzi ni halali

    ReplyDelete
  2. mdau wa kwanza una akili finyu sana

    ReplyDelete
  3. domo jumba la maneno! tanzania hatuna vifaa wala jeshi la kuweza kupigana na uingizaji wa madawa ya kulevya. Kutahitajika uwekezaji wa mamilioni ili kuweza kuhimili vita hivi.

    ReplyDelete
  4. Mmh! Hivi wale watu waliotuhumiwa kumbambikizia Mtoto wa Mengi wako wapi vile?

    ReplyDelete
  5. wewe mdau wa pili ndio akili finyu mwenzako kakupa upana wakufukiria zaidi. anaglia madhara ndio umtukane mwenzako. kwani hatujui mabillionare wengi wanafanya biashara hizi???usitake kuacha wat wazungumze mambo hatari hapa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...