Mtaalamu wa masafa ya Mawasiliano katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Bwana Ikuja Jumanne akimpa maelezo Rais Jakaya Mrisho Kikwete jinsi mitambo ya kudhibiti mawasiliano inavyofanya kazi wakati wa Ufunguzi wa jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA).Kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma na watatu kushoto ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa na mwisho kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano TCRA Bw. Innocent Mungi.
Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) lililofunguliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika barabara ya Sam Nujoma jijini Dar leo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) katika barabara ya Sam Nujoma jijini Dare s Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa na kulia ni Mkurugenzi mkuu wa TCRA Prof.John Nkoma







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Juhudi za "Mtoto Wa Mkulima" za kupiga vita uvaaji wa suti umekwama kabisaaaa.
    Jamaa hawa wanapiga suti za bei mbaya sana.
    Kwa taarifa yako tu ni kwamba suti kumi za hawa jamaa ni sawa na Landcruiser moja lenye mkonga.

    Kiberiti Upele, Katavi Region.

    ReplyDelete
  2. Wewe kiberiti upele, ina mana landcruiser mkonga ni milioni 4 au 5?

    ReplyDelete
  3. mkonga wa mawasiliano wa baharini..umefikia wapi? mbona gharama za internet bado ziko juu..tena zimepanda....hasa dodoma, mwanza...pia spidi bado kabisa...jamani tunaomba mtusaidie...inawezekana wafanya biashara wanahujumu..

    ReplyDelete
  4. HIVI NDUGU ZANGU WATANZANIA SWALA LA MKONGE LIMEFIKIA WAPI??? MBONA RAIS ALILITOLEA HOTUBA NZURI SANA ILIYOJAA MATUMAINI!!!!! KWAMBA ITAPUNGUZA GARAMA ZA MAWASILIANO KWA 93% NA ITAKUWA NA SPEED SANA. MANA KAZI KUBWA YA KUUPITISHA BAHARINI WAZUNGU WAMEFANYA KWA HARAKA NA WALIMALIZA, SASA KAZI RAHISI YA NCHI KAVU AMBAYO UNACHIMBA HATA NA JEMBE HATUJUI IMEFIKIA WAPI NA MWAKA UMEISHA ILA BADO KIMYA, NA HUDUMA ZA MAWASILIANO BADO ZIPO JUU, INTERNET NDIO = NA HAKUNA KABISA TANZANIA. NASHINDWA KUELEWA MAMBO YANAFANYIWA VIPI KAZI TANZANIA. HAKUNA KITU KINACHONIGUSA KAMA HICHI.

    ReplyDelete
  5. Huyo mdau wa 0350 hapo juu hajui kuwa watu tunavaa suti za USD 2000-3000? Huyu anaishi wapi?hivi suti inauzwa laki 4?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...