Dear Michuzi,

Airtel tunaungana na watanzania wote katika kuwapa pole waanga wote wa tukio la mlipuko wa mabomu katika kambi ya jeshi huko Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam.

Tukiwa kama kampuni ambayo siyo tu kwamba tumejidhatiti katika kuleta mawasiliano nafuu kwa watanzania, bali pia tumedhamiria kutimiza wajibu wetu kwa kuhakikisha kuwa mawasiliano na taarifa muhimu zinawafikia walengwa na wadau wote, wakati wote.

Katika dhamira yetu ya kuendelea kusaidia jamii, hasa wale walioathirika na janga hili, tayari tumeshachukua hatua za dhati kuhakikisha kuwa umma, wateja wetu, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wadau wote wanapata fursa kutoa na kupokea taarifa walati wote.

Hatua ya kwanza ni kuwezesha kuwepo namba ya kupiga simu bure “Toll Free” – 188, ambayo imewekwa mahsusi kwa ajili ya wananchi kuitumia kuwasiliana na jeshi la polisi ili kuweza kutoa taarifa ya kupotea au kutoonekana ndugu, jamaa au rafiki kufuatia milipuko ile. Pia namba hii imeweza kutumika na wananchi kuweza kulifahamisha jeshi la polisi juu ya kuonekana mabaki ya mabomu ama vitu vyovyote vyenye kutiliwa mashaka katika makazi ya watu.

Pia tumetoa namba maalum 15526 kwa ajili ya kusaidia waanga wa maafa ya Gongo la Mboto kwa njia ya sms. Watanzania wote wanaweza kuchangia shilingi 500 kwa kila SMS kwa kutuma neon SAIDIA au HELP kwenda namba 15526 ambapo pesa zote zitakazopatikana zitapelekwa katika kuwasaidia waanga wa mabomu.

Wasalaam,

Muganyizi Mutta

Meneja Uhusiano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...