Bw. Richard Goodhead ambaye ametembea kutoka Cape Town Afrika Kusini mpaka Moshi akiwasili kwenye hoteli ya Keys kwa ajili ya kujiandikisha kushiriki mbio ndefu za kilomita 42 za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika kesho Moshi mjini. Richard alianza safari tarehe moja Oktoba mwaka jana na safari yake imetumia muda wa miezi mitano na nusu.
Bw. Richard Goodhead akiwa amepozi kwa picha mara baada ya kuwasili mjini Moshi tayari kwa kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon.
Bw. Richard Goodhead ambaye ametembea kwa miguu kutoka Cape Town Afrika Kusini mpaka Moshi akijiandikisha kushiriki mbio ndefu za kilomita 42 za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika kesho Moshi mjini muda mfupi baada ya kuwasili Moshi mjini. Richard alianza safari tarehe moja Oktoba mwaka jana na safari yake imetumia muda wa miezi mitano na nusu.Na Dixon Busagaga,Moshi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hee Bwana Richard hongera sana kwa kuwa na moyo na uvumilivu ambao umekufanya ukafanikiwa katika lengo lako.

    Watanzania tusome na kujifunza katika hili ni kwamba ukiwa mvumilivu basi mwisho utakula mbivu.

    ReplyDelete
  2. Ama kweli huyu bwana ni "Good-head". Kudunda toka Souzi hadi Bongo si mchezo. Hopefully, pasipo shaka alitembea asije akawa anajitafutia ujiko tu na hukufanya lolote.
    Tutapenda kujua vituko vyake katika Mbio hizo za Kilimajaro.

    ReplyDelete
  3. jamaa alipitia njia gani??maana matembezi ya africa noma.kuna vibaka,snake na simba.mimi nina mpango wa kutoka dar to mwanza lakini kwa baiskeli.kama kuna mdau ana tips zozote anipe

    ReplyDelete
  4. Jamaa yuko feet ni ndani ya miezi mnne alyopiga kwata kutoka south, kweli penye nia pana njia.Na humo mbuganni wanyama wote hao, tena wengine wakali. kama simba,na wengine

    ReplyDelete
  5. Ni umbali wa km ngapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...