Mshambuliaji wa timu ya Bongo Freva,Ali Kiba akijaribu kutaka kumtoka beki wa timu ya Bongo Movie katika mtanange wa Kuchangia maafa ya Gongo La Mboto uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar.Bongo Freva iliibuka kidedea kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimyani na mshambuliaji H. Baba katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Kiungo wa Bongo Movie,Ben Kinyaiya akipiga penati na kukosa kwa kupiga nje.
Mshambuliaji wa kushoto wa timu ya Bongo Freva,KR Mullah akimtoka mchezaji wa timu ya Bongo Movie katika mchezo uliopigwa jioni hii katika uwanja wa Taifa.kwa picha zaidi
BOFYA HAPA.


Ile kesi ya meya wa moshi kumzabua mgambo kwa kufanya kazi yake iko hatua gani vile?
ReplyDelete