MILIPUKO MIKUBWA SANA USIKU HUU IMEIKUMBA JIJI LA DAR KATIKA MAENEO YA GONGO LA MBOTO INAYOSADIKIKA KUWA NI MILIPUKO YA MABOMU KATIKA MOJA YA KAMBI ZA JESHI LA WANANCHI (JWTZ) ILIOPO MAENEO HAYO.
CHANZO CHA MILIPUKO HIYO MPAKA SASA HAKIJAJULIKANA NA RIPOTA WA GLOBU YA JAMII ANAENDELEA KUFUATIA TULIO HILO LINALOENDELEA MPAKA HIVI SASA NA KULIFANYA JIJI LA DAR KUZIZIMA KWA MSHANGAO NA SIMANZI ZA HAPA NA PALE.
TUTAENDELEA KUFAHAMISHANA HALI ITAKAVYOKUWA KATIKA TUKIO HILO KADRI TAARIFA ZA RIPOTA WETU ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA.HIVYO TUVUTE SUBIRA ............
CHANZO CHA MILIPUKO HIYO MPAKA SASA HAKIJAJULIKANA NA RIPOTA WA GLOBU YA JAMII ANAENDELEA KUFUATIA TULIO HILO LINALOENDELEA MPAKA HIVI SASA NA KULIFANYA JIJI LA DAR KUZIZIMA KWA MSHANGAO NA SIMANZI ZA HAPA NA PALE.
TUTAENDELEA KUFAHAMISHANA HALI ITAKAVYOKUWA KATIKA TUKIO HILO KADRI TAARIFA ZA RIPOTA WETU ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA.HIVYO TUVUTE SUBIRA ............
Mume wangu na familia wamenipigia simu niko ughaibuni imewabidi wakimbie nyumba bado wako njiani na ananambia wananchi wasio na magari wanakanyaga wakielekea wasokujua. na tuko Kitunda just imagine. Mbona nchi yetu ni kama ina laana. Tumemkosea nini Mungu Jamani. Kwa nini mabomu wasiyapeleke kwenye kambi za porini yanakaa sehemu kama gongo la mboto ilojaa makazi ya watu. Hapa nilipo nimechanganyikiwa nalia maana hubby ananambia anga lote jekundu na tuna watoto wawili wadogo.
ReplyDeleteMungu Atunusuru!
ReplyDeleteMimi nadhani ina haja ya kuandamana serikali ituhakikishie usalama wetu maana sasa imezidi. Yaani hawajajifunza toka mbagala. Maanake na hivi majeshi yako kila mahali mpaka upanga tutegemee nini. Usalama wa rahia ni kazi ya msingi ya serikali yoyote inayochukua kodi.
ReplyDeletetunaomba kila la kheri katika hali tuliyokuwa nayo...
ReplyDeleteInauma sana . Hii nchi jamani. Kwanini hatujifunzi??????
ReplyDeleteThis is more than too much, hivi watu tukiandamana watasema tunavuruga amani??
Haya mabomu tena,ilikuwa mbagala na sasa gongo la mboto.Kazi kwenu wanajeshi wetu,hii ni kazi yenu kuweza kujua chanzo cha mabomu hayo na mtupe sababu na matokeo yote ya uchunguzi wenu.Siyo tuanze kusikia mara imeundwa tume kushughulikia swala hili wakati ni kazi ya jeshi.Tujaribu kuepukana na mambo haya ya kutumia tume ili kutatua matatizo yetu,hizi tume husababisha mzunguko mkubwa hatimaye kutopata suluhu ya mambo mengi hapa bongo,pia tume ni chazo kingine kinacho sababisha gharama isiyo na sababu,badala ya wahusika ku deal na tatizo moja kwa moja,ushauri wangu ni kuwa tume zipungue bongo hapo ndipo tutafika tuendako.
ReplyDeleteJ.M.Dodoma.
Poleni sana ndugu zangu. Mungu aibariki TZ. This is become too common of an issue. Haven't learned from Mbagala? First of all, The military needs to investigate this and take all the necessary actions kwa uzembe huu. Secondly, the military needs move all the bombs from highly populated areas to remote unpopulated areas. This is crazy.
ReplyDeleteHuu sasa imekuwa uzembe; hii ni mara ya tatu ili suala kutokea nchini. Watu inabidi wawajibishwe. - Mdau(Wichita, Kansas).
ReplyDeletethe Lord is our shield
ReplyDeletemungu wangu...jamani issa tupostie wenzako matumbo yanatuuma tuliokuwa njee ya nchi...jamani ndugu zetu
ReplyDeleteAu ya misri, algeria, libya, yemen na iran yamehamia tanzania! Tuombe dua na mungu atatulindia amani yetu
ReplyDeleteAsiwajibike mtu hapo kabisa.
ReplyDeleteWatanzania tushikamane kujaribu kuwasaidia ndugu zetu kwa hali na mali. Ni lazima tuipe nguvu zaidi kikosi cha uokoaji. Mdau, DZ
ReplyDelete"Dk" JAKAYA KIKWETE, RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO.[UKIWA KAMA MWANAJESHI MSTAAFU] HAYA MABOMU MARA YA KWANZA ILIKUWA BAHATIMBAYA, LAKINI SASA HIVI TUNAHITAJI "UKWELI/UWAZI" KUHUSU MILIPUKO HII...."JE YANAYONENWA NI KWELI" ?
ReplyDeleteEee Mungu ee, Tukimbilie wapi Watanzania siee.Mheshimiwa Raisi tupo chini ya miguu yako Baba,tusaidie watanzania tuishi kwa amani ktk nchi yetu,Tumia sauti yako na cheo chako ili uzinusuru familia za Watanzania wako,Tunajua unawapenda watanzania wote,sasa wakati umefika Baba tunakuombea sana katika wakati huu mgumu. Mungu Ibariki Tanzania
ReplyDeletePoleni sana wahanga wa maobomu ya Gongolamboto.
ReplyDeleteYaani ng'ombe wa maskini hazai, ni juzi tu yametokea Mbagala, watu wengine hata fidia bado hawajalipwa na walikuwa wakiilalamikia serikali, mara kwingine tena kumeitika,,,
Kwa picha hii nadhani yanapeana zamu tusubiri, Lugalo, Kunduchi nk,,,,,
Kama tukio la kwanza hatukupata somo la kujifunza sijui itakuwaje sasa.
Hivi tukiwaomba wahusika wakuu kujiuzulu wawapishe wengine tutakosea?
Tusubiri sasa nini watatueleza,,
Inashangaza kabisa kusikia mtu anadhiriki kusema eti anawapa pole wale wote walioumia na kupoteza maisha. Sidhani kama hili linaingia akilini kwa kweli. Hakuna kiongozi hata mmoja ambae amejitokeza kuzungumzia jambo hili, inaonekana ni jinsi gani hawawajali wananchi wao. Watu wameathirika sijui watafidiwa vp kwani ile ya mbagala ilikuwa ya kiaina, lazima waangalie wale wote waliokuwa wanamiliki nyumba na wale wote waliokuwa wapangaji wa nyumba hizo kwani kila mtu amepoteza kitu muhimu ikiwa ni pamoja na maisha.
ReplyDeleteJamani sasa hii serikali yetu imezidi kwa uzembe, mimi najua jukumu la kwanza la serikali ni kulinda raia wake, iweje leo yenyewe ndio inahatarisha.
ReplyDeletetunaomba tuelezwe kulikoni, huu ni uzembe wa hali ya juu kwani issue ya mbagala ilitokea muda si mrefu, kwann seriklai haikujifunza na kuchukua tahadahri janga kama lile lisitokee tena,
hapa ukitazama na kufikiri kwa makini nahisi kuna agenda ya siri, nahisi kunahujuma hapa wanataka kutoa attention ya watu kwenye "Dowans" kwani hata wakati wa mabomu ya Mbagala Dowans ilikuwa hot sana.
watanzania mko wapi?viongozi, wasomi sasa inabidi tusimame kidete kutetea haki zetu, serikali yetu imeshidwa kutuhakikishia usalama wetu.kwa wale mnaoshi karibu na kambi za jeshi ni muhimu kuchukua tahadhari
NI WAKATI SASA WA KAMBI ZILIZOBAKI KUFANYIWA UCHUNGUZI LA SIVYO ITAKUWA ZAMU KWA ZAMU.WANAJESHI WETU WANAJUA LA KUFANYA KUHUSU MABOMU HAYA.WAWAJIBISHE TU MAANA WAMESOMEA KAZI HII,TENA WAMESOMESHWA NA SERIKALI KWA KODI ZA UMMA.IWEJE UMMA HUU KUANGAMIA KILA WAKATI.
ReplyDeleteNdugu zangu hii hali inatisha isikieni tu kwenye vyombo vya habari. Tuliokuwa karibu hali ilikua mbaya sana,mitikisiko ilikua mikubwa sana, Mabomu yalikua yanapita kama rockets!. Serekali lazima ifanye jitahada za ziada kuepukana na hii hali. Mungu tusaidie. GD Mdaue Kitunda
ReplyDeleteMIPANGO MIJI WANABOMOA NYUMBA ZA WATU WALIOJENGA MABONDENI KWA UONEVU TU. KWA NINI WASIBOMOE MAKAMBI YA JESHI AMBAYO YAMETUZUNGUKA KILA MAHALI. UPANGA KUNA KAMBI YA JESHI, KUNDUCHI, MLALAKUWA, MBAGALA, KILWA ROAD, LUGALO. WATU WANAJENGA SHOPPING MALLS (SHOPPING CENTER) KUZUNGUKA MAKAZI YA WATU SIYO MAKAMBI YA JESHI. HAYA MAMBO YA UJAMAA YAMEPITWA NA WAKATI. BORA HATA WANGEJENGA VITUO VYA POLISI KUZUNGUKA JIJI LETU. MAKAMBI YA JESHI MJINI KWENYE MAKAZI YA WATU NI MAWAZO MGANDO. MAMA TIBAIJUKA ANABOMOA NYUMBA ZA WATU KWA UONEVU, MAKAMBA NAYE NA MABOMU NAYO. SERIKALI NZIMA IMEJIPANGA KUBOMOA NYUMBA ZA WATU. SASA WATANZANIA TUTAISHIJE JAMANI. SERIKALI INABOMOA MPAKA NYUMBA ZA IBADA ULIONA WAPI? MAMBO YA UONEVU HULETA LAANA KWA WATU WANAO UMIZA WENZAO BILA SABABU.
ReplyDeleteMCHUNGAJI`
Huu ni uzembe wa hali ya juu, wa kulaumiwa ni Serikali!
ReplyDeleteNilifikiri kuwa tukio la mbagala lingeleta mabadiliko katika kambi za jeshi na utaratibu mzima wa uhifadhi wa mabomu lakini ni tofauti kabisa na hisia hizi za wengi kwanini mabomu hayo yahifadhiwe karibu na mrundikano wa nyumba nyingi kama gongo la mboto au mbagala leo kwao kesho kambi zingine pata picha kama yataripuka katika kambi za airwing iliyopo karibu na uwanja wa ndege ama kambi iliyopo karibu na uwanja wa uhuru na Mwl Julius K. Nyerere?
ReplyDelete