
Pichani kati ni Afisa Mradi Mwandamizi CHAMPION,Bwa.Yeronika Mlawa akionyesha kadi maalum zitakazogawiwa kwa wageni waalikwa, mbele ya waandishi wa habari ( hawapo pichani) leo jijini Dar,kwenye siku ya maadhimisho yao ya siku ya Wapendanao katika minajili ya uboreshaji wa afya ya jamii kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali waalikwa katika hoteli ya Monen Pick.Maadhimisho hayo pia yatahusisha kujadili pamoja changamoto ambazo wenza/wanandoa Watanzania wanazokutana nazo katika ngazi ya mtu binafsi,familia,jamii na taasisi na namna ambavyo wanaweza kukabiliana nazo kwa kutumia mbinu na mikakati shirikishi.Aidha shughuli hiyo itaendana sambamba na maonyesho ya picha zenye hadithi fupi za wanandoa wa mfano waliochaguliwa na jamii katika wilaya 11 pamoja na kutazama filamu mbili ambazo zinaonyesha wananawake na wanaume wakielezea uzoefu wao katika mahusiano kwenye maisha yao.Shoto ni Afisa Mradi CHAMPION-Dr Katanta Lazarus nakulia kwake ni Afis Mradi Bi.Rose Mtui.

Baadhi ya Waandishi wa habari wakisikiliza mkutano wa mradi wa CHAMPION uliofanyika leo asubuhi jijini Dar kuhusiana na maadhimisho yao ya siku ya Wapendanao katika minajili ya uboreshaji wa afya ya jamii kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali waalikwa ,yatakayofanyika katika hoteli ya Moven Pick,siku ya Valentine Day.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...