WAZIRI wa Elimu Dk. Shukuru Kawambwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Rwekaza Mukandara, wakiingia kwenye mkutano huo.
Picha zote na mdau Muhidin Sufian. Habari kamili
BOFYA HAPA
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kwa maono yangu, wanachodai wanafunzi hawa ni kitu cha msingi kabisa, kwani gharama za maisha zimepanda na zinazidi kupanda kila siku. Kwa mfano kama mafuta, umeme, kodi za pango, chakula, mavazi, nauli, maji, vitabu na vitu vyoote vinavyohitajika kwa mwanafunzi kusoma na kuishi vinapanda, kwanini wao wasipandishiwe fedha wanayokopeshwa? Mimi nafikiri tuache siasa na tuje kwenye hali halisi kwa kuangalia ni kwa jinsi gani hii fedha wanayopewa inatosha ama haitoshi. Hawa ni wasomi na inabidi kuwasiliana nao kisomi. Tatizo watu wenye mamlaka ya kutekeleza mahitaji yao wamemezwa na siasa za kipropaganda ambazo zinalitafuna taifa letu kila kukicha. Tafadhali, tuache siasa iendelee kuwa siasa na mambo ya msingi kama haya tuyachukulie kimsingi na kuhakikisha tunayafanyia kazi kisomi kama ambavyo yanahitaji kufanywa. Tutumie vigezo vilivyotumika kupandisha mishahara na marupuru ya mawaziri, wabunge, wafanyakazi na watendaji wote wa serikali kupandisha mikopo ya wanafunzi hawa kwani mathadha ya mfumuko wa bei hayawapati wao tu bali yanampata kila mtanzania ambapo wanachuo hawa ni sehemu ya watanzania hao.
ReplyDeleteSasa kama hawa wataalamu wetu wa baadaye kila mara wapo kwenye migomo wakifutana chuo kimoja baada ya kingine, taifa letu la baadaye litakuwaje. Wasomi wetu wataweza kushindana na mataifa mengine ambao wasomi wao wanatumia muda mwingi kugundua biofuel, high speed trains, super computer, green-house-gas, and other technological advancement? watoto wetu wanashinda njaa maskini, sijui kama hata wanawaelewa waalimu wao? Hii ni sababu mojawapo ya matokeo mabaya shule za sekondary maana hapo wapo watakaokuwa waalimu baadaye.Kama wao wanasoma kwa matatizo nini tunategemea watakapowafundisha wadodo zao?Hao makandarasi wanaosoma bila kula,barabara zetu na majengo yatakuwaje? Na wale wa Muhimbili niliwahi kusikia wanagoma, inawezekana ndiyo sababu wagonjwa wengi wanakimbilia India kwa kuwakimbia 'stressfull' medical doctors wasomi wa muhimbili wasije pasuliwa kichwa badala ya goti? Nina uchungu sana na hao watoto na nina maswali mengi kuliko majibu, ngoja niishie hapa tu.
ReplyDeletetatizo wanazimega hela za wanafunzi mpaka basi ukija mishahara ya waalimu wanaila vile vile tunaelekea wapi jaman,TZ hatutendewi haki kabisa sasa tumezinduka kama malaria ngoja 2015
ReplyDelete