WAZIRI wa Elimu Dk. Shukuru Kawambwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Rwekaza Mukandara, wakiingia kwenye mkutano huo.
Mpango mzima....
RICHARD Mwita, mmoja wa wanafunzi akihamasiha wenzake kuhakikisha akifika Dk. Kawambwa anatoa tamko tu la nyongeza ya sh. 10,000
Oyaaaaa....tunataka teni
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akiwahutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo mchana, wakati alipokutana nao leo Chuoni hapo kwa ajili ya kusikiliza malalamiko yao. Mara tuu baada ya mkutano zogo kubwa likaumuka na wanafunzi hao walitawanywa na askari kwa kutumia mabomu baada ya kuanza kuwashambulia askari kwa mawe na chupa za maji kutokana na hasira za kutopewa majibu yanayoridhisha kuhusu madai yao.
Sehemu ya umati wa wanafunzi wa UDSM mkutanoni hapo
Sehemu ya umati wa wanafunzi hao wakiwa eneo la mkutano.
Picha zote na mdau Muhidin Sufian. Habari kamili
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwa maono yangu, wanachodai wanafunzi hawa ni kitu cha msingi kabisa, kwani gharama za maisha zimepanda na zinazidi kupanda kila siku. Kwa mfano kama mafuta, umeme, kodi za pango, chakula, mavazi, nauli, maji, vitabu na vitu vyoote vinavyohitajika kwa mwanafunzi kusoma na kuishi vinapanda, kwanini wao wasipandishiwe fedha wanayokopeshwa? Mimi nafikiri tuache siasa na tuje kwenye hali halisi kwa kuangalia ni kwa jinsi gani hii fedha wanayopewa inatosha ama haitoshi. Hawa ni wasomi na inabidi kuwasiliana nao kisomi. Tatizo watu wenye mamlaka ya kutekeleza mahitaji yao wamemezwa na siasa za kipropaganda ambazo zinalitafuna taifa letu kila kukicha. Tafadhali, tuache siasa iendelee kuwa siasa na mambo ya msingi kama haya tuyachukulie kimsingi na kuhakikisha tunayafanyia kazi kisomi kama ambavyo yanahitaji kufanywa. Tutumie vigezo vilivyotumika kupandisha mishahara na marupuru ya mawaziri, wabunge, wafanyakazi na watendaji wote wa serikali kupandisha mikopo ya wanafunzi hawa kwani mathadha ya mfumuko wa bei hayawapati wao tu bali yanampata kila mtanzania ambapo wanachuo hawa ni sehemu ya watanzania hao.

    ReplyDelete
  2. Sasa kama hawa wataalamu wetu wa baadaye kila mara wapo kwenye migomo wakifutana chuo kimoja baada ya kingine, taifa letu la baadaye litakuwaje. Wasomi wetu wataweza kushindana na mataifa mengine ambao wasomi wao wanatumia muda mwingi kugundua biofuel, high speed trains, super computer, green-house-gas, and other technological advancement? watoto wetu wanashinda njaa maskini, sijui kama hata wanawaelewa waalimu wao? Hii ni sababu mojawapo ya matokeo mabaya shule za sekondary maana hapo wapo watakaokuwa waalimu baadaye.Kama wao wanasoma kwa matatizo nini tunategemea watakapowafundisha wadodo zao?Hao makandarasi wanaosoma bila kula,barabara zetu na majengo yatakuwaje? Na wale wa Muhimbili niliwahi kusikia wanagoma, inawezekana ndiyo sababu wagonjwa wengi wanakimbilia India kwa kuwakimbia 'stressfull' medical doctors wasomi wa muhimbili wasije pasuliwa kichwa badala ya goti? Nina uchungu sana na hao watoto na nina maswali mengi kuliko majibu, ngoja niishie hapa tu.

    ReplyDelete
  3. tatizo wanazimega hela za wanafunzi mpaka basi ukija mishahara ya waalimu wanaila vile vile tunaelekea wapi jaman,TZ hatutendewi haki kabisa sasa tumezinduka kama malaria ngoja 2015

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...