JK akikagua mahindi yanayouzwa katika soko la kimataifa la mazao la Kibaigwa wilayani Kongwa,mkoa wa Dodoma leo asubuhi.Kwa mujibu wa uongozi wa soko hilo katika kipindi cha miaka sita kuanzia 2004 hadi 2010 soko hili limeweza kupokea tani za mazao 532,854 na kusafirisha tani 529,143 za mazao tofauti.
JK akiangalia mahindi katika soko la kimataifa la mazao la Kibaigwa wilayani Kongwa,mkoa wa Dodoma leo asubuhi. JK akiongea na wafanyabiashara na wananchi katika soko la Mazao la Kibaigwa lililopo wilaya ya Kongwa,mkoani Dodoma leo asubuhi wakati aliposimama kwa muda sokoni hapo kukagua na kujionea hali halisi ya upatikanaji wa mazao na uhifadhi wa mazao sokoni hapo.

Mwaka 2006 wakati wa ziara yake katika soko hilo Rais alitoa agizo la kutoanika mazao chini ili kulinda afya ya mlaji. Agizo hili limetekelezwa vyema na sasa mazao yanahifadhiwa vyema kuzingatia kanuni za afya. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.


















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...