Ally Ogaga mwenye jeraha mguuni, mgonjwa wa mwisho wa maafa ya maandamano ya Arusha akiwa mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kutoka hospitali jana, pembeni ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha, Elifuraha Paul Mtowe (mwenye suti nyeusi) na Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa (suruali nyeupe na koti Jeusi) walipokuwa wanaongea na waandishi wa Habari mara baada ya mgonjwa huyo kuruhusiwa, wengine ni Diwani wa Viti Maalum Chadema, Bibi Sabina na Katibu wa Mbunge Arusha Mjini Gervas Mgonja. Picha na Habari na Arusha Mambo.

Mgonjwa wa mwisho wa maafa ya Arusha yaliyotokana na maandamano ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ally Ogaga, mkazi wa Moshono Arusha ameruhusiwa kutoka Hospitalini jana baada ya hali ya jeraha la risasi mbili katika mguu wake kuanza kutengemaa.

Muhanga huyo akizungumza katika tukio hilo amekishukuru Chama cha Chadema, Wananchi, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini na Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha kwa ushirikiano waliouonyesha wakati wote aliokuwa akipatiwa matibabu katika Hospilai ya Mount Meru na baadae katika Hospitali ya Seliani zote za mjini Arusha.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba akizungumza katika tukio hilo amesema madhara yaliyompata Ally ni matokeo ya matumizi mabovu ya madaraka na vyombo vya dola dhini ya wananchi, amesema chama hicho kimetimiza ahadi iliyoitoa ya kuhakikisha wahanga wote wa maafa hayo wanapatiwa matibabu na uangalizi wa karibu ili kuhakikisha kuwa wanarejea katika shughuli zao za kawaida za ujenzi wa Taifa.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeo ya Jimbo la Arusha (ArDF) Elifuraha Paul Mtowe amesema Taasisi hiyo imekuwa ikisimamia kwa karibu mahitaji yote muhimu ya wahanga hao na jana imelipa kiasi cha Shilingi Milioni Mbili na Laki Mbili kama gharama za matibabu ya Ally ikiwa ni jitihada za kuhakikisha anaweza kurejea katika shughuli zake za kila siku.
Amesema fedha hizo zilizolipwa zimetokana na michango ya watu mbalimbali wa jimbo la Arusha, Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Wafanyabiashara na Chama chenyewe cha Chadema.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Aman Golugwa ameihakikishia familia ya muhanga huyo kuwa Chama cha Chadema kitaendelea kusaidia na kufuatilia kwa karibu matibabu ya Ally yaliyosalia kama ilivyoelekezwa na daktari, amesema Ally na wahanga wengine wameonyesha moyo wa kijasiri wenye lengo la kutetea haki na kukataa ukandamizwaji.

Hata hivyo Ally ambaye ni mfanyabiashara wa madini mjini Arusha, ameliomba Jeshi la Polisi kumsaidia kupata kiasi cha Shilingi Milioni Mbili na Laki Saba anazodai kunyang’anywa na Polisi mara baada ya kupigwa risasi, amesema alipigwa risasi ya kwanza ya mguu na kuanguka katika mtaro akiwa eneo la Hospitali ya St. Thomas ambako ni eneo lake la kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...