Habari njema sana kwa wanamichezo wa kike, pamoja na wamiliki wa vilabu vya michezo vinavyo wahusisha wanamichezo wanawake.
MAISHAMEMA Tanzania ( MAMET ) tunatoa ufadhili kwa wanamichezo wa kike nchini Tanzania.. Michezo tunayo ifadhili ni ( 1 ) Mpira wa miguu wa wanawake ( 2 ) Mchezo wa masumbwi wa wanawake , pamoja na ( 3 ) Mchezo wa mieleka wa wanawake.
Kama wewe ni mmiliki wa timu ya mpira wa miguu ya wanawake na unahitaji kupata ufadhili wetu, tuma barua yako ya maombi ya ufadhili. Pamoja na barua yako, ambatanisha wasifu kamili wa timu yako pamoja na wasifu wa kila mchezaji katika timu yako na
Kama wewe ni mwanamasumbwi wa kike, ama mcheza mieleka wa kike, na unahitaji kupata ufadhili wetu, tafadhali tuma barua yako ya maombi kwetu, ukiambatanisha maelezo ya wasifu wako kamili pamoja na picha zako.
Maombi yatumwe kwa
Mkurugenzi Mtendaji
MAISHAMEMA Tanzania ( MAMET )
S.L.P 35967
DAR ESSALAAM.
Email: maishamema@gmail.com
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 16/03.2011.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...