Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal, akimfariji Bibi Regina Mshihiri pamoja na Watoto wake Slevia Iddi na Salavina Iddi waliolazwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu kutokana na kuumia vibaya na milipuko ya mabomu iliyotokea juzu usiku kwenye Ghala la kutunzia silaha katika Bohari Kuu ya JWTZ 511KJ Gongo la Mboto jijini Dar es salaam, wakati Mama Bilal alipotembelea Hospitalini hapo leo kwa ajili ya kuwafariji majeruhi hao.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal, akimfariji Mwanajuma Jumaane mkaazi wa Gongo la mboto, aliyelazwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu kutokana na majeraha ya milipuko ya mambomu iliyotokea juzi kwenye Ghala la kutunzia silaha katika Bohari Kuu ya JWTZ 511KJ Gongo la Mboto Dar es salaam, wakati Mama Bilal alipotembelea Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwafariji majeruhi ha leo.
Mke wa Makamu wa Rais wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal, akimfariji Fatma Ali mkaazi wa Gongo la Mboto aliyelazwa wodi ya wanawake katika Hospitali ya Amana kwa matibabu, kutokana na majeraha ya milipuko ya mabomu iliyotokea juzi kwenye Ghala la kutunzia silaha katika Bohari kuu ya JWTZ 511KJ Gongo la Mboto Dar es salaam, wakati Mama Bilal alipotembelea katika Hospitali hiyo leo kwa ajili ya kuwafariji majeruhi hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Michuzi naomba utoe taharifa hii hewani uokoe maisha ya raia. Mimi nakaa maeneo ya Buyuni Pugu kwenye mradi wa serikali. Mabomu yametapakaa maeneo mengi ya hapa. Kuna moja limechimba mbele ya nyumba yetu. Kuna matano nimeyaona kwa macho maeneo jirani. Na kuna mapori mengi hivyo inawezekana mengine hatuwezi yaona. Tumetoa taharifa kwa wanajeshi (tulikutana nao Kajiungeni) wakatupa majibu ya kukatisha tamaa. Wanasema hapo walipo wanaokota mabomu na yamejaa kwenye gari. Hawakuomba namba yetu ya simu wala kuuliza vizuri mabomu yako wapi. Na ujuavyo huwezi bishana na wanajeshi. Tumebaki tunasubuli kufa maana hii ni siku ya pili. Hata kama labda kuna uhaba wa wataalamu wa mabomu, ni mara kumi serikali iombe msaada kuliko kuhacha watu wake tuangamie. Usiporusha hii habari kwenye blog yako damu yangu nikifa itakuwa juu yako. Nia yangu ni msaada si kulaumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...