Mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Group, Yusuph Manji (kulia) akiongozana na Katibu wake, Bw. Muhingo Rweyemamu, wakiingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kuwasilisha vielelezo na kutoa ushahidi katika kesi yake dhidi ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi. Katika kesi hiyo Manji alimtaka Mengi kumlipa fidia ya Sh 1 tu pamoja na kumuomba radhi kupitia Televisheni yake ya ITV kwa muda wa siku saba mfululizo. Picha na mdau Mussa Mateja.

MFANYABIASHARA maarufu jijini Dar es Salaam na mdhamini wa Yanga, Yusuf Manji, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kwamba yeye sio Fisadi Papa kama alivyotuhumiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Reginald Mengi.

Aidha alidai tuhuma zote zilizotolewa na Mengi kwamba yeye ni mnyonyaji wa watu wa hali ya chini, anahusiana na Dowans, Richmond, rada ya jeshi tuhuma zote ni uzushi hazina ukweli wowote.

Akitoa ushahidi leo mbele ya mahakama hiyo akiongozwa na wakili wake, Mabere Marando, alidai tuhuma za Mengi zimemshushia heshima yake kwenye jamii wakati yeye ni mtu ana heshimiwa na baadhi ya watu wanamfanya ‘role model’ wao kwamba siku moja wawe na mafanikio kama yeye.

Manji alidai kufuatia kauli aliyoitoa Mengi kupitia vyombo vya habari anavyovimiliki imesababisha aonekane mtu asiyefaa katika jamii na katika familia yake na familia inataka kumtenga kwasababu haina imani nae tena.

Kesi hiyo ni kesi iliyofunguliwa na Manji ambayo anadai fidia ya Shilingi 1/- (moja tu) kwa madai ya kudhalilishwa na Mengi kupitia vituo vyake vya Televisheni na kwenye magazeti.

Manji alidai kuwa klabu ya Mpira wa miguu ya Yanga kufuatia heshima yake imemteua kuwa mfadhili, aidha alionyesha baadhi ya barua ambazo zilikuwa zikimpa mualiko katika shudhuli mbali mbali za kizamii ikiwapo ya mualiko wa maafali ya kumaliza shule wanafunzi wa kidato cha sita shule ya Benjamini Mkapa, jijini.

Kesi hiyo iko mbele ya Hakimu Aloyce Katemana Manji anawakilishwa na mawakili Mabere Marando, Beatus Malima, Dk. Ringo Tenga na Richard Rweyongeza.

Manji alionyesha ushahidi wa picha za video ambayo ilionyeshwa mahakamani ikimuonyesha Mengi akiwatangaza Manji na wafanyabiashara wengine kuwa ni mafisadi papa.

Manji akiulizwa kuhusu tuhuma za kuwa na nyumba Amerika na Afrika ya Kusini akidai kwamba hana nyumba yoyote aliyoinunua ndani au nje ya nchi nyumba zote ni za baba yake ambaye alifariki na kumuachia mama yake.

Alidai nyumba hizo kuna baadhi mama yake alimpa kama zawadi na hata anayoishi ni ya baba yake ambaye sasa ni marehem.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Huyu an utani na sh. Moja ya Mangi?

    ReplyDelete
  2. He, anadai fidia ya sh. moja? hebu angalia hapa naona umekosea

    ReplyDelete
  3. kiboko yake...one shilling!!!

    ReplyDelete
  4. yaani mangi hatoi hata chilingi

    ReplyDelete
  5. manji, ukimshinda mengi wapo wengine waja, tarajia

    ReplyDelete
  6. Manji wants to prove a point (if he has one) sio kudai fidia.

    ReplyDelete
  7. Jamani manji ni handsome acha tu na mihela juuu mmmmmh!

    ReplyDelete
  8. fanya utafiti kidogo, pata kuelewa maana ya madai ya shs 1

    ReplyDelete
  9. kuchafua hali ya hewa maana yake nini kama sio kujamba??

    ReplyDelete
  10. Jamani manji ni handosome sura yake safiiiiiiiii no makovu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...