






Warembo hao leo wamefanya Ziara ya Kihistoria katika Hifadhi ya Mikumi ambapo walifika katika Vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika hifadhi hiyo ikiwemo, mabwawa ya Viboko yaliyosheheni Viboko wakubwa wanaofiki ukubwa wa zaidi ya Nusu tani, wakiwa sambamba na Mamba wakubwa wenye nguvu na urefu wa zaidi ya mita 10.
pia warembo walijionea makundi makubwa ya tembo, Twiga, Nyati, Pundamilia, Swala, Pofu, Mbwa Mwitu, na zaidi ya aina mia nne za ndege wakubwa kwa wadogo.
katika ziara hiyo warembo walipokewa na kaimu mhifadhi wa Mikumi National park Apaikunda Mungure ambaye alielezea kufurahishwa na ujio wa warembo hao ambao alisema kuwa watasaidia sana kutangaza hifadhi hiyo ya taifa.
katika ziara hiyo Miss Utalii Kagera Daissy Mushumbusi mwenye Digrii ya kwanza ya utalii kutoka chuo kikuu cha Moi alinyakua Tuzo ya kuwa barozi wa utalii wa hifadhi ya Taifa ya Mikumi na kuwabwaga warembo wengine 47 wanaoshiriki shindano hilo.
Leo warembo wanaendelea na ziara katika hifadhi ya taifa ya Udzungwa.
Naona wanachukua notes. Ingefaa kila moja aaandike insha kuhusu walichooana. Ingesaidia katika selection process.
ReplyDeleteHapo akiibuka mnyama mkali inakuwaje? Shule inaendelea ama vipi?
ReplyDelete(US Blogger)
Dah kweli nimefurahishwa na hawa mamiss, eti wanavaa gloves za hospitali kwenye kazi ya zege...kwani hawajui kuna gloves za zege na hizo walizovaa?
ReplyDelete