Waziri wa uchukuzi Mh.Omari Nundu akionyesha jina lake mara baada ya kuweka jiwe la msingi la karakana la matengenezo ya ndege za shirika la precision air lililopo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere anaeshudia ni Mkurugenzi mtendaji wa Precision Air Alfonse Kioko
Waziri wa uchukuzi Mh.Omari Nundu kushoto akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa mambo ya usalama wa Precision air Allan Sharra(katikati)wakati wa kuweka jiwe la msingi la karakana la matengenezo ya ndege za shirika la precision air lililopo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere,kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Precision Air Alfonse Kioko.


Waziri wa Uchukuzi Mh. Omari R. Nundu leo ameweka jiwe la msingi la karakana la matengenezo ya ndege la shirika la ndege la Precision lilopo uwanja wa ndege wakimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Dar es Salaam.

Ujenzi wa karakana hiyo umegarimu Dola za Kimarekani 5.4 milioni ulianza Aprili 2010 na unatarajiwa kuisha mnamo March mwaka huu. Karakana hilo inauwezo wakuingia ndege tatu za aina ya ATR72, B767 au Airbus 330 kwa maramoja. Karakana hilo ndiyo litakuwa lenye uwezo mkubwa wa matengenezo yote ya ndege za aina ya ATR Afrika mashariki na kati.

Karakana hilo pia itakuwa na uwezo wakutengeza ndege zote za shirika la Precision pamoja na ndege za mashirika mengine yatakayohitaji huduma zake zikiwemo za C- check. Shirika linatarajia kuajiri watanazania wengi zaidi ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi wa idara yake ya matengezo ya ndege.

Ujenzi wa karakana hilo unafanywa na kampuni ya M/s Catic International Engineering (T) Ltd, kwa mkopo unaotolewa na Kenya Commercial Bank.
Kampuni ya ndege ya Precision imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja wake kwa kutumia vifaa vyake vipya na vya kisasa katika soko la biashara ya ndege.

Mnamo mwaka 2006 Kampuni ya Ndege ya Precision na kampuni ya kutengeneza ndege ya ATR walisaini mkataba wa Dola milioni 129 kwa ajili ya ununuzi wa ndege saba mpya katika mpango wake wa kuboresha ndege zake. Ndege ya mwisho kutoka ATR iliwasili Jijini Dar es Salaam mwezi Septemba mwaka jana.

Mkataba huu wa kibiashara wa ndege hizi saba (2 ATR 42-500 na 5 ATR 72-500) iliwezesha Precision Air kutunukiwa zawadi mbili za kimataifa. Mwezi Aprili 2009, Jarida la AirFinance lilizawadia mkataba huu kuwa Mkataba wa kibiashara bora zaidi kwa Afrika katika mwaka 2008.

Mkopo huo wa ndege za ATR ulizawadiwa Desemba mwaka juzi na Gazeti la Usafirishaji Jane's Finance, kama "Mkopo mkubwa wa mwaka Afrika wa ndege 2008."

Kuletwa kwa ndege hiyo ya mwisho mwezi Septemba imefanya kampuni hii ya ndege kuwa na jumla ya ndege kumi, saba kati ya hizo ni mpya kabisa. Kampuni ya Precision Air pia inatumia ndege moja aina ya Boeing 737.

Kampuni hii ya ndege ina mtandao mkubwa wa safari za anga ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara. Kampuni ya Precisionair pia hufanya safari zake za anga katika miji ya Nairobi na Mombasa nchini Kenya na Entebbe nchini Uganda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Halafu Tanzania inaendelea kusupport au kutaka kufufua ATC? Ni tatizo kubwa. Ni wakati mwafaka kwa sasa tukaichukua Precision air na kuifanya National carrier period. Ni ya Watannzania, walianza kama wajasiriamali, hao sasa wanafanya mambo ambay ATC ni ndoto. Serikali think Big, and after all serikali haitakiwa kufanya biashara. why ATC????

    ReplyDelete
  2. Precision wakiendelea hivi.. watafunika sana.. maana wako 'siriaz' kweli kweli. Ryanair ilianza na kindege kiduunchu.. sasa hivi wana ndege 260+ na orders kibao. Safi sana., hii inadhibitisha serikalini kuna ukiritimba wa hali ya juu kwani ATC hadi leo kimeo

    ReplyDelete
  3. Wala serikali wasiiguse kabisa Precision maana wataiua tu nayo kama ATC.Mara ya mwisho nilisikia kuwa 49% ni Kenya Airways na 51% ni watanzania. Na ndio maana connection nyingi,kama sio zote, za Kenya Airways/KLM pale Nairobi kuja Dar zinafanywa na Precision.
    Yaani ukitaka kuamini kuwa serikali wanacheza na ATC,hebu chungulia website ya Kenya Airways;
    www.kenya-airways.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...