Ningependa kuwataarifu kwamba kutakuwa na mkutano wa mwaka(AGM) wa Jumuia ya Watanzania wote wanaoishi Namibia. Kama mnavyofahamu, ni muda mrefu tangu tumekuwa na mkutano kama huu.

Hivyo ni muhimu kwa kila Mtanzania kadiri inavyowezekana kuhudhuria na kushiriki katika mkutano kupanga mustakbali wa Jumuia yetu.

Mkutano utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 5 Februari, saa nane(8) mchana nyumbani kwa Bw Manyama Maregesi, Klein Windhoek, bila kuchelewa, ili tuweze kumaliza shughuli zetu kabla ya saa 12 jioni. Naomba swala la muda lizingatiwe.

Kila mmoja wetu ni mdau katika jambo hili, hivyo kila Mtanzania afanye juhudi ya kuhudhuria kikao hiki muhimu. Siwezi kusisitiza vya kutosha juu ya kuwahi.

Wenu katika ujenzi wa Taifa

John Gabone

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...