MBUNGE wa Jimbo la Vunjo Mh. Augustino Lyatonga Mrema amewashangaa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kushindwa kuafikiana kuhusu kuungana na vyama vingine kuunda kambi ya upinzani bungeni.


Akitoa hoja bungeni jioni hii mjini Dodoma leo jioni Mh. Mrema amesema kuwa anawashangaa CHADEMA kwani yeye ndio alipaswa kuwa kiongozi wa kambi hiyo kwa kuwa alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali nyeti katika awamu tofauti.


“Kwanza mimi ndio nilipaswa kuwa Kiongozi wa kambi ya upinzani kwa sababu nimeshawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri mkuu, nimewahi kuwa Mbunge katika majimbo matatu tofauti na vyama tofauti, nimegombea urais mara tatu na sasa hivi ni Mbunge.


“Huo ufisadi wanaosema wameufichua wamebabia tu. Ufisadi ulikuwepo siku nyingi. Mimi nilifichua ufisadi wa Chavda na ndege iliyobeba dhahabu....hawa wanasema nini sasa hivi....Mimi nimeshawahi kufukuzwa bungeni wao wamefukuzwa lini na nani??? Wanatoka nje tu,” alisema Mh. Mrema.


Hata hivyo Mh. Mrema alizuiliwa kuendelea kuongea na Spika wa Bunge Anne Makinda kwa kuwa muda aliopewa kutoa hoja ulikuwa umemalizika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Du choka mbaya!!!

    ReplyDelete
  2. anawakilisha akili za watu wa Marangu! Tutaona mengi haki!

    ReplyDelete
  3. huyu mzee anaelewa siasa vizuri,kwa kweli sasa chadema naona wanaanza kupotea kwenye siasa.wanachochea vurugu na ugomvi hawafai
    ningekua uwezo wangu ningekifutilia mbali hichi chama.KWANINI KINAHATARISHA AMANI YA UMMA?wanakosa hoja za msingi

    ReplyDelete
  4. Bahati mbaya sana kama ndio wazee wa aina hii tuliobaki nao - na bado wanalipwa mishahara na posho za ubunge kutoka katika mfuko wa walipakodi!!!!!

    ReplyDelete
  5. inasikitisha sana kuona watu walioaminiwa na wananchi wao kupewa dhamana
    yakuwakilisha bungeni wamebakia kulumbana wakati wananchi wakiendelea
    na umasikini wa kutupa,ujinga,maradhi,elimu duni,ukosefu wa umeme
    ambao sasa umeleta athari kubwa ya uchumi wa wanyonge walio wengi.
    kuna mambo mengi ya msingiyakuongea bungeni.
    na huu ni udhaifu mkubwa wa viongozi wetu wengi wa kiafrica
    nasema hili kwa uchungu sana sana sana.
    ni juzi tu nasikiliza idhaa ya kiswahili ya bbc london
    waziri mmoja wa burundi anataka kupeleka mswada bungeni WAKUTOJAMBA hadharani,sasa hapo ndo utapima kama hayo ni maendeleo au ujinga
    NAWASHAURI WABUNGE WATIMIZE MATARAJIO YA WALIOWACHAGUA KULIKO
    KUENDELEZA MABISHANO YASIOKUWA NA TIJA KWA WANANCHI

    ReplyDelete
  6. ...Ankal...Nina maswali kadhaa ambayo ningependa kuelimishwa na wasomaji wa globu ya jamii.. Hivi chama cha Mhe. Mrema kina wabunge wangapi katika bunge la sasa? Kwa idadi yao wanatengeneza asilimia ngapi ya wabunge wote? Je kwa idadi hiyo, wanatosha kuanzisha kambi ya upinzani bungeni kwa mujibu wa kanuni za bunge? Ni hayo tu, naombeni kuelimishwa!

    Mdau wa Mwenge!

    ReplyDelete
  7. huyu nae hana sera kwanza haelewekagiiiiiiiiiiiii,badala azungumzie kuhusu umeme maana imekuwa kero ye vijembe.

    ReplyDelete
  8. Chadema wana hoja ya msingi - utaundaje kambi ya upinzani na partner ambaye ni nusu ccm nusu upinzani?
    Kuhusu mrema ni bora angepewa masurufu yake akapumzike na nafasi yake akapewa mtu mwingine. Wananchi wa Vunjo mmeumia kwani sidhani ana la kuwatetetea bungeni. Unaongelea CV ya kubahatisha badala ya performance!!!

    ReplyDelete
  9. Michuzi naomba kuchangia hivi-

    - Kwanza mbona unasema "Chadema wamechafua hewa", umepata wapi jumuisho hilo? Kiongozi wa blog unaweka mawazo yako kuwa kichwa cha mjadala? Unaaminisha umma kuwa kilichofanyika ni makosa.

    - Pili, Mrema anakosea sana. Naposema aliibua maswala ya kina Chavda na wizi wa dhahabu, hatukatai. Sasa anataka Chadema wasiendelee na vita dhidi ya ufisadi kisa yeye alishaianzisha miaka mingi? Mbona aliyeanzisha kupiga ufisadi si yeye kama ni hivyo, angalia Nyerere alifanya nini, angalia Sokoine alifanya nini, nk.

    - Tatu, Watanzania tusishabikie umiliki wa bunge kwa chama cha CCM tukadhani watu kutoka nje ni upumbavu. Wangepigana ngumi ndani kwa kutokubaliana ndio utaratibu? Kumbukeni ccm ndio wengi na wana maamuzi yenye hasara mengi tu. Chadema wasipoungwa na upinzani wengine, tunakokwenda ccm wanatutupa jalalani.

    - Mwisho, ningependa kuuliza maswali ya msingi CCM, kama umeme tu hawjamaliza tatizo, maji, ambayo yakikushinda unaweka mwekezaji, nalo wameshindwa pia. Wana haja gani ya kuendelea kutudanganya wanatuongoza? Hivi tunajua ni wangapi wanakufa kwa kukosa huduma za msingi nchi hii? Achilia mbali kuinua nchi kiuchumi kwa jumla.

    ReplyDelete
  10. Mzee wa Kiraracha bwana!

    ReplyDelete
  11. JAMANI MREMA, Uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuwi, nleka njiende nlaone

    ReplyDelete
  12. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WABUNGE WAKE, NCHI IKAUMBWE UPYA NA WABUNGE WAPYA. TUNAOAMINI KATIKA MWISHO WA DUNIA, NDIO HUU. KAMA BUNGE LINAWEZA KUTUKANA HADHARANI, BASI TUMEKWISHA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...