Akitoa hoja bungeni jioni hii mjini Dodoma leo jioni Mh. Mrema amesema kuwa anawashangaa CHADEMA kwani yeye ndio alipaswa kuwa kiongozi wa kambi hiyo kwa kuwa alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali nyeti katika awamu tofauti.
“Kwanza mimi ndio nilipaswa kuwa Kiongozi wa kambi ya upinzani kwa sababu nimeshawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri mkuu, nimewahi kuwa Mbunge katika majimbo matatu tofauti na vyama tofauti, nimegombea urais mara tatu na sasa hivi ni Mbunge.
“Huo ufisadi wanaosema wameufichua wamebabia tu. Ufisadi ulikuwepo siku nyingi. Mimi nilifichua ufisadi wa Chavda na ndege iliyobeba dhahabu....hawa wanasema nini sasa hivi....Mimi nimeshawahi kufukuzwa bungeni wao wamefukuzwa lini na nani??? Wanatoka nje tu,” alisema Mh. Mrema.
Hata hivyo Mh. Mrema alizuiliwa kuendelea kuongea na Spika wa Bunge Anne Makinda kwa kuwa muda aliopewa kutoa hoja ulikuwa umemalizika.
Du choka mbaya!!!
ReplyDeleteanawakilisha akili za watu wa Marangu! Tutaona mengi haki!
ReplyDeletehuyu mzee anaelewa siasa vizuri,kwa kweli sasa chadema naona wanaanza kupotea kwenye siasa.wanachochea vurugu na ugomvi hawafai
ReplyDeleteningekua uwezo wangu ningekifutilia mbali hichi chama.KWANINI KINAHATARISHA AMANI YA UMMA?wanakosa hoja za msingi
Bahati mbaya sana kama ndio wazee wa aina hii tuliobaki nao - na bado wanalipwa mishahara na posho za ubunge kutoka katika mfuko wa walipakodi!!!!!
ReplyDeleteinasikitisha sana kuona watu walioaminiwa na wananchi wao kupewa dhamana
ReplyDeleteyakuwakilisha bungeni wamebakia kulumbana wakati wananchi wakiendelea
na umasikini wa kutupa,ujinga,maradhi,elimu duni,ukosefu wa umeme
ambao sasa umeleta athari kubwa ya uchumi wa wanyonge walio wengi.
kuna mambo mengi ya msingiyakuongea bungeni.
na huu ni udhaifu mkubwa wa viongozi wetu wengi wa kiafrica
nasema hili kwa uchungu sana sana sana.
ni juzi tu nasikiliza idhaa ya kiswahili ya bbc london
waziri mmoja wa burundi anataka kupeleka mswada bungeni WAKUTOJAMBA hadharani,sasa hapo ndo utapima kama hayo ni maendeleo au ujinga
NAWASHAURI WABUNGE WATIMIZE MATARAJIO YA WALIOWACHAGUA KULIKO
KUENDELEZA MABISHANO YASIOKUWA NA TIJA KWA WANANCHI
...Ankal...Nina maswali kadhaa ambayo ningependa kuelimishwa na wasomaji wa globu ya jamii.. Hivi chama cha Mhe. Mrema kina wabunge wangapi katika bunge la sasa? Kwa idadi yao wanatengeneza asilimia ngapi ya wabunge wote? Je kwa idadi hiyo, wanatosha kuanzisha kambi ya upinzani bungeni kwa mujibu wa kanuni za bunge? Ni hayo tu, naombeni kuelimishwa!
ReplyDeleteMdau wa Mwenge!
huyu nae hana sera kwanza haelewekagiiiiiiiiiiiii,badala azungumzie kuhusu umeme maana imekuwa kero ye vijembe.
ReplyDeleteChadema wana hoja ya msingi - utaundaje kambi ya upinzani na partner ambaye ni nusu ccm nusu upinzani?
ReplyDeleteKuhusu mrema ni bora angepewa masurufu yake akapumzike na nafasi yake akapewa mtu mwingine. Wananchi wa Vunjo mmeumia kwani sidhani ana la kuwatetetea bungeni. Unaongelea CV ya kubahatisha badala ya performance!!!
Michuzi naomba kuchangia hivi-
ReplyDelete- Kwanza mbona unasema "Chadema wamechafua hewa", umepata wapi jumuisho hilo? Kiongozi wa blog unaweka mawazo yako kuwa kichwa cha mjadala? Unaaminisha umma kuwa kilichofanyika ni makosa.
- Pili, Mrema anakosea sana. Naposema aliibua maswala ya kina Chavda na wizi wa dhahabu, hatukatai. Sasa anataka Chadema wasiendelee na vita dhidi ya ufisadi kisa yeye alishaianzisha miaka mingi? Mbona aliyeanzisha kupiga ufisadi si yeye kama ni hivyo, angalia Nyerere alifanya nini, angalia Sokoine alifanya nini, nk.
- Tatu, Watanzania tusishabikie umiliki wa bunge kwa chama cha CCM tukadhani watu kutoka nje ni upumbavu. Wangepigana ngumi ndani kwa kutokubaliana ndio utaratibu? Kumbukeni ccm ndio wengi na wana maamuzi yenye hasara mengi tu. Chadema wasipoungwa na upinzani wengine, tunakokwenda ccm wanatutupa jalalani.
- Mwisho, ningependa kuuliza maswali ya msingi CCM, kama umeme tu hawjamaliza tatizo, maji, ambayo yakikushinda unaweka mwekezaji, nalo wameshindwa pia. Wana haja gani ya kuendelea kutudanganya wanatuongoza? Hivi tunajua ni wangapi wanakufa kwa kukosa huduma za msingi nchi hii? Achilia mbali kuinua nchi kiuchumi kwa jumla.
Mzee wa Kiraracha bwana!
ReplyDeleteJAMANI MREMA, Uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuwi, nleka njiende nlaone
ReplyDeleteMUNGU IBARIKI TANZANIA NA WABUNGE WAKE, NCHI IKAUMBWE UPYA NA WABUNGE WAPYA. TUNAOAMINI KATIKA MWISHO WA DUNIA, NDIO HUU. KAMA BUNGE LINAWEZA KUTUKANA HADHARANI, BASI TUMEKWISHA
ReplyDelete