Kaka Michuzi.

Kwanza, pole kwa kazi nzito na nzuri ya kuhabarisha watanzania duniani kote. Mimi binafsi nimekuwa addicted na blogu yako kwa kupata habari za nyumbani ukizingatia kuwa tuko mbali na nyumbani.

Blog yako inatufanya wengi wetu kujisikia kuwa tuko karibu na nyumbani.
Pili, tumeshuhudua jinsi blogu yako inavyoweza kwa njia moja au nyingine kutafuta suluhisho kwa baadhi ya mahitaji bila ya kuwa na mipaka.

Kwa misingi hiyo, ninakuomba unisaidie kutundika tangazo hili kwa minajili ya kumtafuta rafiki yangu aitwaye Verediana Anthony Kuzenza.

Verediana amekuwa rafiki yangu tukiwa wadogo Nzega - Tabora, lakini kwa bahati mbaya tulipoteza mawasiliano pale nilipokwenda High School 1994.

Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mawasilino maana sikujua yeye alipokwenda. Nimejaribu kutafuta habari zake, inaonekana kuwa amejiunga 2011 na Chuo cha Utumishi kilicho chini ya ofisi ya Rais (Tanzania Public Service College).

Kwa sasa inaniwia vigumu kumtafuta kwa sababu sina contacts zake na mimi mwenyewe niko nje ya Afrika.

Nitashukuru sana iwapo utanisaidia kwa hilo.

Anaweza kunipata kwa njia ya email zebsung@yahoo.com

Natanguliza shukrani kaka na kukutakia siku njema.

Zebinah Masunga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mangi wa KiboshoFebruary 17, 2011

    Alishaolewa na ana watoto 5.ninayo simu yake lakini sikupi maana mumewe ana wivu sana.Tulia na wako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...