HABARI KAKA MICHUZI NA WAPENZI WA BLOG YA JAMII KWA UJUMLA.

NAPENDA KUWAARIFU KUWA LEO ASUBUHI MAMA YANGU MZAZI
MRS MWAJUMA MAGANGA"MAMA MAGANGA AMEFARIKI DUNIA
NYUMBANI MAGOMENI MAPIPA MTAA WA KIYUNGI KITUO CHA MOROCCO HOTEL

MAZIKO YATAFANYIKA LEOLEO NYUMBANI MAGOMENI,NILIKUWA NAOMBA UNIWEKEE TAARIFA HIZI ILI ZIWAFIKIE WANA NDUGU NA JAMAA POPOTE PALE WALIPO ILI KUTAMBUA JUU YA MSIBA HUU MZITO AMBAO SINA JINSI YA KUUELEZEA.

KWA KUWA NIPO MBALI NA NYUMBANI(TZ) NAOMBA UNIPEPERUSHIE HABARI HII TAFADHALI KWANI NINA IMANI KUPITIA BLOG YA JAMII HABARI ZITAWAFIKIA WENGI,MAZIKO YATAFANYIKA BAADA YA KUSALI SAA KUMI JIONI.

Kwa niaba ya Familia nzima,
Maganga One (Ughaibuni)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Pole sana mdau wa ughaibuni kwa kuondokewa na Mama mzazi, hakika huo ni msiba mkubwa hasa ukikupata ukiwa mbali na nyumbani.
    Sasa je, unahitaji mchango wowote mbali na kutupa taarifa?? Je, unategemea kwenda nyumbani kwa ajili ya msiba huo au mambo ya 'makaratasi' hayajakaa sawa??
    Kama hujapata makaratasi, chonde chonde vumilia huko huko ughaibuni kwani nyumbani hali ni ngumu sana kwa watu ambao hawamo katika 'mtandao'

    Inna Lillah Wainna Ilayhu Rajiuuun.

    Abiola Jr. - columbus, OHIO

    ReplyDelete
  2. Pole sana taarifa tulizipata hapa tangu asubuhi na tuliwasiliana nao Tanzania pamoja na mdogo wako MRISHO anaeishi MWANZA ambaye nae amewahi kumkuta MAMA MAGANGA katika hatua za mwisho kabla umauti haujamkuta.Na tumejitahidi kuzisamabaza taarifa za msiba kila kona ya ulimwengu huu kwa wanaokujua.Pole sana MZEE MAGANGA kwa kuondokewa na mzazi wa pili,yote kazi ya MUNGU.

    ReplyDelete
  3. Pole sana kaka yangu. Mungu atakusaidia katika kipindi hiki kigumu na tumuombee mama mapumziko ya amani. We love you mum but god loved you more.

    ReplyDelete
  4. INNAA LILLAAHI WAINNAA ILAYHI RAAJIUUN.
    ALLAH AMSAMEHE NA KUMREHEMU MAMA YETU.
    Hakika ni msiba mkubwa kaka, ALLAH AWAPE SUBIRA NA KUWALIPA KWA MSIBA HUU.
    Hakika kama sikutembelea hii blog nisingepata taarifa, bila shaka mdogo wako Mrisho Haroun Maganga ameghafilika kutujulisha wadau wake, na hii ni kutokana na mshtuko na kutingwa na mipangilio ya mazishi.
    Nduguyo Dr. Hussein J A

    ReplyDelete
  5. innallilah wainna ilayhi rajiun.. pole sana Maganga One kwa kufiwa na mzazi wako.

    ReplyDelete
  6. Pole sana Maganga One. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. May she Rest in Eternal Peace.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...