Shirika la Umeme nchini, Tanesco, limenunua mafuta ya kuendeshea mtambo wa umeme wa IPTL uliopo Tegeta, Dar es Salaam, ili kuzalisha megawati 80 kwa siku, ikiwa ni moja ya hatua zake kujaribu kupambana na mgawo wa umeme ambao shirika hilo limekiri kuwa unailipunguzia heshima kwa umma.

Akizungumza na waandishi wa habari , kwenye makao makuu ya Tanesco, Ubungo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Injinia, Felchesmi Mramba,(Pichani), alisema, mafuta yameshanunuliwa na yameanza kuwasili IPTL, ili kuzalisha kiasi hicho cha megawati za umeme kwa siku.

"Hii itapunguza wa umeme kwa sasa kwa megawati zipatazo 70", alisema Injinia huyo ambaye alifuatana na Meneja Uhusiano wa Shirika hilo, Badra Masudi (kulia, Pichani) na kuongeza "tunatarajia kwamba msimu wa mvua za masika utaanza punde, na hii itafanya uzalishaji wa umeme katika mitambo ya maji kuongezeka na hivyo kuliondoa tatizo hilo kwa sasa.

"Pia Shirika linawasiliana na serikali kuangalia uwezekano wa kupata mit ambo ya dharura ili kukabiliana na hali inayoweza kujitokeza endapo mvua za masika zitakuwa chini ya wastani unaotarajiwa", akasema Injinia Mramba.

Akasema, uongozi wa Tanesco unawaomba radhi sanaaaa, wananchi kutokana na usumbufu mkubwa unaotokana na adha ya mgawo huo wa umeme na pia Shirika linawasihi wananchi kushirikiana na shirika hilo, na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha upungufu wa umeme.

"Tunaahidi kwamba tutafanya kila jitihada kurekebisha mapungufu balimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza hapa na pale katika utekelezaji wa zoezi hili la mgawo hasa kudhibiti matukio ya dharura yanayofaya ratiba zisifuatwe kama zilivyopangwa", akamalizia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. TANESCO wana wajibu wa kununua mafuta ya kuendesha Mitambo ya IPTL? Hivi mkataba wa IPTL na TANESCO ukoje? maumivu jamani, hebu tuelewesheni hapo!

    ReplyDelete
  2. hamna maana kabisa ebu kwendeni zenu uko
    ipo siku watu watawajibika kwa huu uhuni kwa wanainchi
    yani unazidi kukukera mnunue mitambo gani mingine ya dharura???????????
    aisee ata msiporudisha kbs umeme na nchi ikaingia gizani ni sawa tu

    mna utani na nchi hii

    ReplyDelete
  3. Mimi ningepata fursa ya kuwa Raisi hata kwa saamoja tu Ningeamuru wakurugenzi wa TANESCO HQ na Bodi yao waswekwe ndani segera na madaraka yao wakiwa nayo na vikao vya utatuzi wa tatizo la umeme TZ wavifanyie huko No alowances No any pay as they have had enough by now na solution za kudumu wanazo ila makusudi yaliyo pea na ubinafsi na tamaa kuu zimewafanya kuona hapo ndipo pa kuganga njaa zzao za ziada..... zisizoisha.... mbona nji jirani japo wna migao ila kunaeleweka jitihada zinzofanyika na pia bei za umeme ni ndogo kuliko kwetu - la ajabu hata huko jirani tunakowauzia huu huu wetu bado bei ni ndogo.... Jamani hapa kunanii??? Misri Oyeeeee.

    ReplyDelete
  4. Hawa jamaa ni wababaishaji tu.... tafiti kadhaa zimeonyesha sehemu kadhaa za nji hii kuna mivumona mikondo ya upepo kwa kipindi chote cha mwaka..... kwanini hao wasomi huko ambao naamini wamesoma sana na wanajua vianzishi vinginewe vya nguvu za umeme wasitumie nguvu ya upepo kuzalisha umeme ??? na kwanini viwanda vikubwa kama vile TPC Moshi wanauwezo wa kuzalisha umeme wa ziada ambao ungeweza kutosha kwa sehemu walo ndogo kama vile mji wa Moshi wasiruhusiwe kuuza umeme hapo??? urasimu huu wa kijinga unatuweka nji nzima katika tatizo moja bila ya lazima.... aibu yenu milele...Ifike mahali wasomi waliosoma kwa ghrama ya walipa kodi wanaposhindwa kazi waondolewe kazini lakini pia sifa na vyeti vyao vifutiliwe mbali..... I am sorry ... inauma sana....

    ReplyDelete
  5. Hayo ni maneno ya kutuliza ball....! hapo ni ulaji mwingine wa kununua hayo mafuta!! hebu waone hapo walivyotakata - wao umeme kwao kibao ama huo wao ama majenereta Injinia kavaa suti kali.... atashughulikia saa ngapi kadhia hii.... wanawaza solution nyepesi za muda na zenye maslahi zaidi kwao binafsi.... Na nyie waandishi wa habari mnaitwa na na mnawasikiliza tena mnakuwa hamnazo mkiwazia bahasha tu!! hamuwaulizi maswali magumu juu ya utatuzi wa kudumu wa shida hii ya aibu .... mnashikishwa mpango 0 mnatoka nao nje baada ya kikao chenye makulaji na feza za dhambi kisha mnakuja tuambia "wananunua mafuta"...We are sick and tired!! of these endless and hopless songs!!by now We Dont Want to know the Process!!! We want stable electricity/Power!

    ReplyDelete
  6. Bure Tu!! Tunataka Injinia wavae overalls wakae katika dawati waje na solution za kudumu kwa tatizo hili..... Kama kuna ukame jwabu ni kuwa na jua kwa wingi zaidi na kwa muda mrefu zaidi Je kwanini shirika lisiwe na mkakati wa makusudi kuanzisha mpango kabambe wa kuzalisha umeme kwa nguvu za jua???? ndiyo mipango ya kutaifa na siyo ya kuita waandishi na kuwaambia habari nyepesinyepesi ambazo hazitutoi katika janga hili... zaidi ni gharama zidi na kwa maana hiyo bei juu zaidi.... Lakini pia umeme upelekwe kwa wadau na wananji wengi zaidi ili uchangiaji ushirikishe wengizaidi na kwa hiyo bei nafuu zaidi na kwa hiyo uwezo mkubwa zaidi kwa shirika katika kuendesha na kuendeleza nguvu ya umeme kote Tz.....

    ReplyDelete
  7. Wajibu wa shirika la umeme (Tanesco) ni kutoa huduma ya umeme. How they will provide that service its up to them. Mtumiaji wa umeme (consumer) hana haja ya kujua kampuni ya umeme anayoilipa kwa sababu huu umeme hautolewi bure unapatikanaje. Management inayolipwa hela nyingi tu kwa kazi ambayo haionekani ndio ilitakiwa ibuni mbinu za kuhakikisha kuwa umeme unapatikana,na unakuwa reliable. Sasa nashangaa Tanesco kuweka press conference kwa kile ambacho kilitakiwa kiwe ni “responsibility” yao in the first place. This is absurd.

    ReplyDelete
  8. Kasahani hako ka 'china' ka nini? Kametoka Asia nini? Si ajabu Malaysia!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...