

Onyesho hilo limepangwa kufanyika februari 11,ndani ya hoteli ya Moven pick,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni sh 20,000/=kwa kila kichwa.Aidha katika onyesho hilo wabunifu mahiri wa mavazi 20 wataonyesha mitindo ya Kitanzania,kwa kuwataja wachache atakuwepo Ally Rhemtullah,Mustafa Hassanal,Manju Msita,Khadija Mwanamboka,Fransisca Shirima,Zamda George,Dayana Magesa,Kemi Kalikawe,Martin Kadinda,Joiyce na wengineo kibao.
Katika onyesho hilo pia kutakuwepo na burudani mbalimbali itakayotolewa,litakuwepo kundi la Babloom taarab,Trio Band,Baby Madaha,kikundi cha ngoma za asili Simba Traditional Dance pamoja na msanii mahiri wa kizazi kipya Chid Benz.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...